Ugumu wa kupima unaongeza maambukizi ya numonia Jamhuri ya Afrika ya Kati: UNICEF

Kusikiliza /

mtoto anayeugua numonia

Kampeni kabambe kupitia vyombo vya habari imezinduliwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati katika juhudi za kuongeza ufahamu kuhusu ugonjwa wa numonia, ambao unaongoza katika kusababisha vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

Kampeni hiyo ambayo imezinduliwa leo kwenye Siku ya Numonia Duniani na Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, likishirikiana na mtandao wa waandishi wa habari kuhusu haki za binadamu, itaangazia dalili za ugonjwa huo, jinsi unavyoenezwa, na unavyotibiwa, pamoja na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kuuzuia.

Pamoja na hayo, kampeni hiyo itaangazia chanjo dhidi ya numonia, ambayo ni sehemu ya mpango wa kina wa utoaji chanjo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031