Uamuzi wa Baraza Kuu la UM kwa Palestina ni kichocheo cha amani Mashariki ya Kati

Kusikiliza /

Baraza Kuu

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Balozi Augustine Mahiga amesema uamuzi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa kuipatia Palestina hadhi ya uangalizi bila haki ya kupiga kura katika Baraza hilo, ni hatua muhimu inayochochea mchakato wa amani Mashariki ya Kati.

Balozi Mahiga amesema hayo katika mahojiano na Radio ya Umoja wa Mataifa ambapo ameelezea maana ya hatua hiyo.

(SAUTI YA AUGUSTINE MAHIGA)

Katika kura hiyo ya jana ya kupitisha azimio hilo, nchi 138 ziliunga mkono huku Tisa zikipinga na nchi 41 zikijiondoa katika upigaji kura.

Nchi zilizopiga kura ya hapana ni pamoja na Marekani na Israeli huku Uingereza na Hungary zikiwa miongoni mwa nchi ambazo hazikuonyesha msimamo wowote.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031