Tathmini ya uharibifu nchini Haiti kutokana na kimbunga inafanyiwa majumuisho: OCHA
Kusikiliza /Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA nchiniHaiti, Johan Peleman amesema wanasubiri ripoti ya majumuisho ya tathmini ya madhara yaliyotokana na kimbungaSandykilichopiga nchi hiyo wiki iliyopita ili waweze kufahamu msaada unaohitajika na idadi kamili ya watu walioathiriwa wakati huu ambapo inakadiriwa watu Elfu Ishirini hawana makazi.
Peleman ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa kimbunga hicho kilisababisha watu wengi kuhamishwa ikiwa ni kando ya wale Laki Tatu na Nusu waliokuwa wanaishi kwenye kambi baada ya tetemeko la ardhi la mwaka jana.
(SAUTI YA PELEMAN)
Peleman amesema ni matumaini ya ofisi yake kuwa mwishoni mwa wiki hii itatoa ombi maalum la msaada iwapo itashindwa kukidhi mahitaji.
