Homa ya Marburg yaendelea kusambaa nchini Uganda

Kusikiliza /

Shirika la afya duniani, WHO limesema ugonjwa wa homa ya Marburg umeendelea kusambaa nchini Uganda ambapo hadi sasa watu Kumi na Mmoja wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Wagonjwa 20 wameripotiwa katika wilaya Tano nchini humo ikiwemo kwenye mji mkuu Kampala.

Homa ya Marburg iliripotiwa kulipuka katika wilaya ya Kabale Kusini Magharibi mwa Uganda tarehe 19 mwezi uliopita ambapo Mwakilishi wa WHO nchini humo Dkt. Joachim Saweka anasema mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo inaimarishwa ili usisambae zaidi.

"Hadi sasa hatufahamu kiwango cha mlipuko. Tumeweza kuweka vikosi vyetu katika maeneo mbali mbali ili kuweza kufuatilia ugonjwa huu na ndipo tunaweza kufahamu hali halisi ya mlipuko. Tunaongeza uwezo wetu wa kubaini wagonjwa na kuwafuatilia ili usisambae kwa kasi."

Kwa mujibu wa WHO, tayari nchi jirani na Uganda zimepatiwa taarifa ili zidhibiti mipaka yao na kujiandaa ili kuepusha ugonjwa huo kuingia katika nchi hizo. Hata hivyo shirika hilo la afya duniani limesema hakuna kizuizi chochote cha kusafiri au kufanya biashara na Uganda.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031