Serikali ya Haiti yaomba msaada wa UM baada ya Kimbunga Sandy

Kusikiliza /

kimbunga-sandy

Umoja wa Mataifa umesema kuwa yapata watu milioni 1.6 nchini Haiti wameathirika vibaya sana na kimbunga Sandy, ambacho kilipita pwani ya mashariki mwa Marekani na maeneo ya Karibi wiki moja iliyopita.

Serikali ya Haiti imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa na wafadhili kutoa misaada ya dharura ili kuwasaidia manusura na waathirika wa kimbunga hicho.

Kimbunga Sandy kilisababisha uharibifu mkubwa katika maeneo kilipopita, ukiwemo makazi na huduma muhimu kama za umeme, huku kikiripotiwa kuwaua zaidi ya watu hamsini kote nchini Haiti.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031