Sekta ya Viwanda yataka mfumo wa UNFC utumike kwa vyanzo asilia vya nishati

Kusikiliza /

vyanzo asilia vya nishati

Watalaamu kuhusu nishati asilia wamesema kuna umuhimu wa kuwa na mfumo mmoja na wa uwazi zaidi wa kutathmini na kufahamu idadi ya vyanzo asilia vya nishati kwa uwazi wakati huu ambapo sekta hiyo na nishati asilia inakuwa ya kibiashara zaidi.

Jopo la wataalamu hao lilikuwa na mkutano huko London, Uingereza kwa siku tatu kuanzia tarehe 31 mwezi uliopita ambapo walikubaliana kuwa mfumo wa Umoja wa Mataifa wa kuainisha nishati itokanayo na makaa ya mawe, gesi na petroli, hifadhi ya madini na rasilimali, UNFC wa mwaka 2009 unaweza kutumika kubainisha vyanzo asilia vya nishati.

Wamesema matumizi ya mfumo huo yatawezesha ulinganifu wa maana zaidi kati ya vyanzo asili vya nishati na vile visivyo asilia.

Licha ya kwamba uwezekano wa matumizi ya UNFC kwa vyanzo asilia vya nishati ulijadiliwa kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa kundi la wataalamu la tume ya uchumi ya Ulaya mwezi Mei mwaka huu, uwezekano wa kuutumia unajadiliwa kwa kina hivi sasa na jopo la wataalamu wa nishati asilia inayotumika viwandani.

Idadi kubwa ya washiriki wa mkutano huo wa London wametaka kuharakishwa kwa nyaraka ya kuwezesha kutumiwa kwa muundo wa UNFC kwa vyanzo vya nishati asilia.

Warsha ya pili ya kuwezesha kuharakisha mpango huo na kushirikisha wadau wote imepangwa kufanyika robo ya kwanza ya mwaka ujao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031