Raia wa Sudan Kusini walioko Khartoum waanza kurejeshwa Aweil: IOM

Kusikiliza /

raia wa Sudan Kusini warejea nyumbani kwa ndege

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali za Sudan na Sudan Kusini zimeanza kusafirisha raia Elfu Moja Mia Tatu Sabini wa Sudan Kusini kutoka mji mkuu wa Sudan, Kharthoum kwenda mji wa Aweil ulioko jimbo la Bahr El Ghazal, Sudan Kusini.

Raia hao pamoja na familia zao ni wale walioko katika mazingira magumu zaidi na mpango huo unatekekelezwa kwa ushirikiano kati ya nchi mbili hizo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na lile la uhamiaji, IOM.

Mpango wa kusaidia raia hao kurejea Sudan Kusini utafanyika kwa wiki mbili na wanatumia ndege mbili za kukodi. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031