Programu za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi zarejelea tena nchini Mali

Kusikiliza /

kupambana na ugonjwa wa Ukimwi

Mfuko wa kimataifa unaofadhili vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, Kifua kikuu na Malaria hii leo umesaini makubaliano na Shirika la maendelo la Umoja wa Mataifa UNDP ya kurejelea tena programu za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi hasa matibabu ya ugonjwa huo kwa maelfu ya watu nchini Mali.

Kupitia makubaliano hayo mfuko huo uliidhinisha ufadhili wa dola milioni 75 zitakazotumika kutoa matibabu dhidi ya ugonjwa wa ukimwi nchini Mali kwa muda wa miaka mitatu. Kwa sasa karibu watu 50,000 wanaishi na virusi vya ukimwi nchini Mali. Progamu hiyo inalenga watu walio kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa ukimwi na pia katika kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031