Pillay alaani mashambulizi kwenye sehemu za raia kwenye ukanda wa Gaza na Israel

Kusikiliza /

Faixa-de-Gaza

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa ni jambo lisilokubalika kuwa raia ndio wanaondelea kuhangaika kufuatia msukosuko uliopo kati ya serikali ya Israel na utawala wa Palestina.

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa usalama wa raia ni jukumu la pande zote husika kuambatana na sheria za kimataifa. Pillay ameelezea wasi wasi wake kutokana na hali ilivyo katika eneo hilo ambapo amezitaka pande zote mbili kusitisha makubilino yanayoweza kuwa hatari. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

"Kamishna mkuu mara kwa mara amelaani kufyatuliwa kwa makombora kutoka ukanda wa Gaza kwenda kusini mwa Israel na ameelezea wasi wasi wake kufuatia kuongezeka hivi majuzi kwa idadi ya mashambulizi ya makombora yakiwa sasa yanalengwa kwenye mji wa Tel Aviv. Pia ametiwa wasi wasi na kuongezeka kwa mashambulizi ya angani kutoka kwa vikosi vya Israal kwenye eneo lenye watu wengi la ukanda wa Gaza kwa muda wa siku mbili zilizopita ambapo amezita pande husika kujizuia na mashambulizi yaliyo hatari."

 

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031