Ofisi ya haki za binadamu ya UM yashutumu kuhangaisha kwa watu wanaokisiwa kuwa mashoga na wasagaji nchini Cameroon

Kusikiliza /

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi wake kutokana na ripoti za kuhangaishwa, kudhulumiwa, kukamatwa na kufungwa kwa watu wanaokisiwa kuwa wasagaji au mashoga nchini Cameroon. Sheria za sasa nchini Cameroon zinaharamisha uhusiano baina ya watu wa jinsia moja na inaruhusu hadi kifungo cha miaka mitano pamoja na faini.

Sheria hiyo hata hiyo inatajwa kuwa inaenda kinyume na sheria za haki za kibinadamu za Umoja wa Mataifa na inakiuka haki ya kutotengwa. Mwaka 2011 mwanamme mmoja kwa jina Roger Jean-Claude alifikishwa mahakamani kwa kukikishiwa kuwa shoga baada ya kumtumia ujumbe wa mapenzi mwanamme mwingine. Pia kumekuwa na ripoti za kutishiwa maisha watetesi wa haki za binadamu ambao wamekuwa wakitetea haki za mashoga na wasagaji.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031