Nchi wanachama wa WHO zapiga hatua kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Kusikiliza /

Makao Makuu ya WHO

Mfumo wa kwanza wa aina yake duniani wa kufuatialia baadhi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanayoongoza duniani kwa vifo umeridhiwa huko Geneva, Uswisi na nchi wanachama wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO.

Mwenyekiti wa mkutano huo Dkt. Bjørn-Inge Larsen amesema mfumo huo umeweka malengo Tisa na viashiria 25 vya kuzuia na kudhibiti magonjwa hayo kama vile moyo, kisukari, saratani, mapafu na mengineyo.

Pamoja na mambo mengine, rasimu ya mfumo huo inajikita zaidi katika kushughulikia athari za magonjwa yasiyoambukiza kwa kutathmini maendeleo yalofikiwa katika kupunguza magonjwa yahusianayo na magonjwa hayo, vifo na kupunguza mazingira ya kuweza kupata magonjwa hayo.

Dkt. Larsen ametaja mazingira hayo kuwa ni matumizi ya tumbaku, unywaji hovyo wa pombe, lishe isiyo bora na kutokufanya mazoezi.

Mfumo huo utajadiliwa kwenye kikao cha na baraza la utendaji la WHO kitakachofanyika mwezi Januari mwakani na baadaye kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu wa shirika hilo mwezi Mei kwa ajili ya mjadala na kupitishwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031