Mzozo Ukanda wa Gaza; Ban kukutana na viongozi wa Israel na Palestina

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon yuko nchini Misri ikiwa ni sehemu ya ziara yake huko Mashariki ya Kati ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kushughulikia mapigano yanayoendelea hivi sasa huko Ukanda wa Gaza kati ya Palestina na Israel.

Msemaji wa Bwana Ban amewaeleza waandishi wa habari kwa njia ya simu kutoka mji mkuu wa Misri, Cairo kuwa leo Katibu Mkuu anakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri na kesho atakutana na Rais wa Misri.

Amesema kuwa wakati wa ziara hiyo Bwana Ban atakuwa na mazungumzo na viongozi wa Israel mjini Tel Aviv na wale wa Palestina huko Ramallah.

Halikadhalika amesisitiza umuhimu wa pande zote kujizuia na mashambulizi yanayoendelea kuua raia wasio na hatia na watoe fursa kwa mkondo wa amani unaoongozwa na Misri kwa ajili ya kusitisha mapigano.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031