Msaada wa dharura wa chakula unatakiwa Haiti: WFP

Kusikiliza /

WFP, Haiti

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema linahitaji dola Milioni 20 kwa ajili ya msaada wa chakula kwa watu Laki Mbili na Elfu Ishirini na Tano nchini Haiti wanaokabiliwa na matatizo kutokana na kimbunga Sandy kilichokumba nchi hiyo.

Msemaji wa WFP Elizabeth Byrs amesema hivi sasa watu hao wamepoteza makazi yao, mazao na kwamba hali imekuwa mbaya zaidi kwa kuwa kimbunga Sandy kimepiga baada ya ukame na kimbunga Isaac vilivyokumba nchi hiyo mwezi Agosti.

Ameongeza kuwa mara baada ya kimbunga Sandy kupiga Haiti, WFP iliweza kuwapatia msaada wa dharura wa chakula watu Elfu 13 na wiki hii kwa kushirikiana na serikali wamesambaza chakula cha siku 21 kwa familia Elfu 20 zilizopo kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi. Hapa Bi. Byrs anafafanua mahitaji yanayotakiwa zaidi.

“WFP sasa inahitaji na inaomba msaada wa haraka wa zaidi ya dola Miloini 20 kusaidia msaada wa chakula kwa watu zaidi ya 425 nchini Haiti. Ni kwa ajili ya operesheni ya dharura ya kusambaza chakula ikijumuisha mahitaji maalum ya lishe kwa ajili ya zaidi ya  wanawake wajawazito Elfu Moja , wanawake waliojifungua na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Tunahitaji kuwasaidia watu hao katika miezi ijayo na ndio maana hizo dola Milioni Ishirini zinahitajika haraka. Fedha hizo ni sehemu ya ombi la fedha la Umoja wa Mataifa litakalozinduliwa na jumiya ya Umoja huo mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo kusaidia manusura wa kimbunga Sandy nchini Haiti.”

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031