Mkuu wa WFP ahitimisha ziara yake Mashariki ya Kati na kuahidi msaada kwa wakimbizi wa Syria

Kusikiliza /

Ertharin Cousin

Katika hatua nyingine mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP Ertharin Cousin amehitimisha ziara yake ya siku tatu huko Mashariki ya Kati iliyompeleka hadi nchi za Lebanon na Jordan kujionea hali halisi ya wakimbizi wa Syria waliokimbia nchi yao kutokana na mapigano yanayoendelea.

Pamoja na kuzungumza na viongozi, alikutana pia na wakimbizi mathalani katika kambi ya Zaatari iliyoko Jordan ambako wanawake walimweleza madhila waliyopata wakati wakikimbia Syria ikiwemo kujificha nyakati za usiku hadi kuingia Jordan.

Bi. Cousin akizungumza na waandishi wa habari kwenye kambi hiyo amesema anatambua mazingira magumu yanayowapata wakimbizi hao na kwamba WFP imejizatiti kushirikiana na makundi mbali mbali na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kufanya mazingira kuwa bora zaidi.

(SAUTI YA ERTHARIN COUSIN)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930