Mkuu wa IAEA atembelea Iraq

Kusikiliza /

Yukiya Amano

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la linalohusika na nguvu za atomiki Yukiya Amano amekutana na waziri Mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki mjini Baghdad wakati wa ziara yake nchini humo ambayo imekusudia kutoa ujumbe wa pongezi kwa serikali ya nchi hiyo iliyoridhia itifaki ya nyongeza.

Bwana Amano ameisifu serikali ya Baghdad juu ya hatua yake ya kuanza kutekeleza sehemu ya itifaki ya nyongeza na kuongeza kusema kuwa kitendo hicho kinatuma ujumbe wa matumaini katika uso wa dunia.

Wakati wa mkutano wao, pande zote mbili zilibadilishana mawazo na kuelezea haja ya kufanya kazi kwa uwazi na ili kuendelea kufufua matumaini ya wananchi wa eneo hilo.

Kwa upande mwingine, Bwana Amano alimhakikishia Waziri Mkuu Malik pamoja na waziri wake wa mambo ya nje kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono matumizi ya amani ya teknolojia ya nukilia na kusisitiza jumuiya ya kimataifa inapaswa kuelewa utashi na dhamira ya taifa hilo wakati linaanzisha teknolojia hiyo

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031