Mkutano wa WHO kuhusu matumizi ya tumbaku kufanyika Seoul, Korea Kusini

Kusikiliza /

matumizi ya tumbaku

Mkutano wa Shirika la Afya Duniani kuhusu mkataba wa kudhibiti bidhaa za tumbaku unatazamiwa kufanyika mjini Seoul, Korea Kusini wiki ijayo, ukiwa ni mkutano wa tano wa mataifa wanachama wa mkataba huo.

Mkutano huo wa wanachama unatazamiwa kurejelea, kufanyia marekebisho na kuendeleza utekelezaji wa mkataba huo. Inatarajiwa kuwa mwishoni mwa mkutano huo, mkakati wa kwanza wa kutokomeza biashara haramu ya bidhaa za tumbaku utaafikiwa.

Baadhi ya vitu vitakavyozingatiwa kwenye mkutano huo ni maelekezo kuhusu bei na ushuru dhidi ya bidhaa za tumbaku ili kupunguza matumizi, mapendekezo ya sera kuhusu njia zingine za kupata riziki, mbali na kupanda tumbaku, pamoja na masuala ya tumbaku isiyo ya moshi, kama vile ya kutafuna.

Dr. Vijay Trevedi kutoka WHO anasema bara la Afrika ni mojawapo ya maeneo ambapo udhibiti wa bidhaa za tumbaku na matumizi yake upo chini.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031