Mkutano wa kujadili athari za itifaki ya soko la pamoja la EAC kwa uhamiaji kufanyika Tanzania: IOM

Kusikiliza /

nemba ya EAC

Shirika la Kimataifa la uhamiaji kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania wiki ijayo wataandaa mkutano wa mashauriano kuhusu athari za uhamiaji zitokanazo na itifaki ya soko la pamoja la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC.

Mkutano huo wa siku tatu utakaoanza jijini DSM tarehe 13 utajumuisha maafisa wa IOM, na wale wa kutoka wizara za mambo ya ndani na mambo ya Nje za Tanzania pamoja na mamlaka nyingine husika kama ile ya mapato.

Itifaki ya soko la pamoja la EAC ilianza kutumika mwezi Julai mwaka 2012 na inaondoa vizuizi vya biashara, ajira, huduma na mitaji miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo ambazo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29