Mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa wang'oa nanga Qatar

Kusikiliza /

Abdullah Bin HamadAL-Attiyah

Mkutano wa 18 wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa umeng’oa nanga hii leo mjini Doha Qatar. Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo rais wa vikao Abdullah Bin HamadAL-Attiyah amewaambia wanaohudhuria kuwa madadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa kwa ubinadamu na mkutano huo ni fursa muhimu inayostahili kutumika kwa njiia nzuri.

 

Wengine waliozungumza ni pamoja na rais wa mkutano anayeondoka Maite Nkoana-Mashabane na Christiana Figueres, mkurugenzi mkuu wa UNFCCC ambaye amemshukuru rais wa Qatar na wakfu wa nchi hiyo.

 

Mkutano huo utakuwa ndio wa kwa kwanza wa Umoja wa Mataifa ambao hautatumia programu za makaratasi ambapo washiriki watakuwa na uamuzi wa kuchapisha nakala wanazohitaji. Katika hotuba yake, Bi Christiana Figueres amesema kuwa ingawa hatua zimepigwa zaidi katika miaka michache iliyopita katika kuweka ahadi, hatua zaidi zinafaa kuchukuliwa, kuanzia kwenye mkutano wa Doha

(SAUTI YA CHRISTIANA FIGUERES)

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031