Misukosuko yasababisha kuhama kwa watu zaidi nchini DRC

Kusikiliza /

wakimbizi DRC

Kuendelea kuwepo kwa misukosuko kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kumechangia kuongozeka kwa idadi ya watu wanaohama makwao nayo mahitaji ya chakula yakizidi kupanda. Zaidi ya watu 260,000 wamalazimika kuhama makwao kwenye mkoa wa Kivu kaskazini tangu kuanza kwa mzozo mwezi Aprili mwaka huu.

Juma hili shirika la mpango wa chakula duniani WFP lilianzisha shughuli za usambazaji wa chakula kwa wakimbizi wa ndani 14,000 kwenye kambi ya Mugunga eneo la Goma. WFP pia itatoa misaada ya chakula kwa njia ya pesa na Vocha mwezi huu kwa wakimbizi 76,495 kwenye maeneo ya Minova na Bweremana.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031