Mavuno yaongezeka DPRK lakini bado lishe ni duni

Kusikiliza /

mavuno nchini DPRK

Ripoti mpya ya tathmini ya uzalishaji wa chakula huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK iliyoandaliwa baada ya ziara ya maafisa wa Shirika la chakula duniani FAO na lile la mpango wa chakula WFP nchini humo imebaini kuwepo kwa lishe duni miongoni mwa wananchi wa nchi hiyo licha ya ongezeko la mavuno.

Imebainika kuwa watu Milioni Mbili nukta Nane bado wanakabiliwa na ukosefu wa lishe bora kutokana na kutokuwepo kwa mlo wa vyakula vyenye protini na mafuta.

Wataalamu hao walitembelea majimbo Tisa yanayozalisha mazao ya chakula huko DPRK mwezi Septemba na Oktoba ambao ni msimu wa mavuno ya nafaka.

Walionyesha wasiwasi wao wa kupungua kwa kilimo cha maharagwe aina ya Soya pamoja na kuwepo kwa kiwango kidogo cha mboga za majani, hali inayosababisha ukosefu wa viini lishe muhimu mwilini kama vitamini na protini. Marcus Prior ni msemaji wa WFP nchini Thailand.

(SAUTI YA MARCUS PRIOR)

"Licha ya ongezeko hilo, wasiwasi mkubwa wa WFP na Jumuuiya zinazotoa misaada ya kibinadamu ni kwa watoto watoto wadogo ya kwamba wanapaswa kupata lishe bora wanayohitaji kwa siku Elfu moja za mwanzo za hai wao yaani tangu tumboni hadi wanapotimiza umri wa miaka miwili. Bila kupata mlo wa aina hiyo ni sawa na kuwahukumu adhabu ya kifo kwa makuzi yao ya kimwili an kiakili.

Halikadhalika wataalamu hao wamesema ni vyema kuhakikisha wanawake nchini Korea Kaskazini wanapata mlo wenye protini na mafuta wakati wa ujauzito na hata baada ya kujifungua ili watoto wanaozaliwa na wale wanaonyenyeswa wawe na afya bora.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031