Matokeo ya uchunguzi wa yaliyojiri Sri Lanka yatasaidia kuimarisha UM: Malcorra

Kusikiliza /

Susana Malcorra

Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa Susana Malcorra amesisitiza kuwa ripoti kuhusu yaliyojiri nchini Sri Lanka katika miezi ya mwisho ya vita vya wenyewe kwa wenyewe itatumiwa kuimarisha zaidi utendaji wa umoja huo hususani katika kusaidia wale wenye mahitaji.

Bi. Malcorra amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani leo kuhusu ripoti hiyo iliandaliwa na jopo lililoundwa na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon mwaka 2010 kuchunguza nafasi ya Umoja wa Mataifa ikiwemo sekretarieti, mashirika na programu za Umoja huo nchini Sri Lanka, wajumbe wa baraza la usalama na lile la haki za binadamu wakati vita vilipokuwa vinafikia ukingoni.

Amesema Umoja wa Mataifa utatumia mapendekezo ya ripoti hiyo ili kujiimarisha na kutoa huduma bora zaidi.

Ripoti hiyo ilieleza kuwa Umoja wa Mataifa haukughulikia ipasavyo viashiria vya mapema vya hali iliyojitokeza miezi ya mwisho ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sri Lanka.

Hapo jana baada ya kupokea ripoti hiyo na kuiweka bayana kwa umma, Bwana Ban alisema Umoja wa Mataifa umeazimia kujifunza kutokana na yaliyobainika ili kuweza kuhudumia vyema watu hususani wale walio kwenye migogoro.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031