Marekebisho ya Katiba Colombia kuhusu mahakama za kijeshi yaangaliwe upya: UM

Kusikiliza /

ramani ya Colombia

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya haki za binadamu, inamsihi Rais wa Colombia na kiongozi wa bunge la nchi hiyo kuangalia upya mchango wao kwenye marekebisho ya katiba ya nchi hiyo ambayo yanalenga kubadilisha wigo wa mfumo wa mahakama ya kijeshi nchini humo.

Msemaji wa ofisi hiyo Cécile Pouilly amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa wasiwasi ni kwamba iwapo yataridhiwa, marekebisho hayo yatakandamiza jitihada za awali za serikali ya Colombia za kuhakikisha kuwa vitendo vyote vya ukikwaji wa haki za binadamu vinavyofanywa na wanajeshi au polisi nchini humo vinachunguzwa na wahusika wanafikishwa mbele ya sheria.

Pamoja na kueleza kuwa mapendekezo ya sasa yanafanya baadhi ya vitendo vibaya zaidi vya ukiukwaji wa haki za binadamu kuweza kukwepa sheria mbele ya mfumo wa mahakama ya kijeshi, ofisi hiyo inasema kuwa vitendo vingi vya ukikwaji haki vitapatiwa uamuzi kwenye mahakama ya kijeshi ambayo ndiyo itakayoamua kiwango cha uhalifu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930