Mapigano kati ya majeshi ya Sudan na waasi huko Shangil Tobaya yakomeshwe: UNAMID

Kusikiliza /

 

Mlinda amani wa UNAMID

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa Darfur, UNAMID kimeeleza wasiwasi wake kuhusiana na kuendelea kwa mapigano kati ya vikosi vya jeshi la Sudan, SAF na kikundi cha waasi huko Shangil Tobaya na kutaka mapigano hayo yakomeshwe mara moja.

Taarifa ya UNAMID imemkariri Kaimu mwakilishi maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika Aichatou Mindaoudou akiitaka serikali ya SUDAN na vikundi vya waasi kukubaliana kuwa ghasia haiwezi kuleta suluhisho lolote badala yale inaleta madhara kwa wakazi wa jimbo la Darfur.

Halikadhalika amezitaka pande hizo kuheshimu sheria za kimataifa na zile za haki za binadamu na kushiriki kikamilifu katika kutatua mgogoro wa Darfur kwa njia ya amani.

Taarifa hiyo imesema kutokana na ghasia za Ijumaa, UNAMID baada ya kuombwa, iliwasafirisha kwa ndege baadhi ya wapiganaji waliojeruhiwa kwenda El Fasher kwa ajili ya matibabu na UNAMID imekuwa ikitoa msaada huo wa matibabu kwa pande zote bila upendeleo wowote.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031