Makabaliano ya kusitisha mapigano Gaza yanazingatiwa licha ya mauaji ya raia mmoja: UNRWA

Kusikiliza /

Filippo Grandi

Huko Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada kwa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limetoa taarifa kuhusu hali halisi baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya kikundi cha Hamas na Israel na kusema makubaliano hayo yanaonekana kuzingatiwa licha ya mauaji ya mtu mmoja huko Khan Younis eneo lililoko mpakani.

Kwa mujibu UNRWA vijana wa kipalestina waliokuwa wakifurahia makubaliano hayo walikaribia eneo la mpakani na kuweka bendera zao ambapo jeshi la Israeli lilishambulia na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi Kumi na Tisa.

Hata hivyo usambazaji wa vifaa vya msaada unandelea ambapo kati ya tarehe 23 na 24 zaidi ya watu 200 kutoka mashirika mbali mbali wakiwemo madaktari waliingia Gaza kutoa msaada.

Wakati huo huo Kamishna mkuu wa UNRWA Filippo Grandi ametaka jumuiya ya kimataifa na pande kwenye mgogoro huko Gaza kutumia fursa itokanayo na makubaliano ya kusitisha mapigano .

Akizungumza na tume ya ushauri ya UNRWA, Grandi ameviita vizuizi vyote vya Israeli huko Gaza kuwa si halali na kutaka viondolewe ikiwemo vile vya kutembea, uvuvi na biashara.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031