Katibu Mkuu ataka Syria na Israel ziepuke mzozo wa aina yoyote kwenye milima ya Golan

Kusikiliza /

unpatrolgolan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametaka pande zote kwenye mzozo wa milima ya Golan kujizuia kufanya mashambulizi wakati huu ambapo walinzi wa amani wa Umoja huo wanaendelea kusimamia mkataba wa mwaka 1974 wa kusitisha mapigano kati ya Israeli na Palestina.

Ametoa wito huo kufuatia taarifa kuwa mapigano kati ya majeshi ya Syria na kikundi cha upinzani nchini humo yalichochea Israeli kujibu mapigo.

Bwana Ban ametaka Syria na Israel kuacha mara moja urushaji wowote wa kombora katika eneo la milima ya Golan linalosimamiwa na makubaliano ya mwaka 1974.

Habari zinasema kuwa kombora moja lililotokana na mapigano kati ya majeshi ya Syria na yale ya upinzani, lilitua kwenye kituo cha kijeshi cha Israeli kwenye milima ya Golan siku ya Jumapili, jambo lililochochea Israeli kurusha kombora la onyo kwenye eneo la Syria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2014
T N T K J M P
« mac    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930