Jitihada za kusambaza misaada Syria zilifanikiwa kwa kiasi licha ya changamoto: UNHCR

Kusikiliza /

UNHCR yatoa msaada kwa watu wa Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema wakati wa sikukuu ya Eid El Adha lilifanikiwa kwa kiasi fulani kuwasilisha misaada ya kibinadamu kwa baadhi ya maelfu ya familia nchini Syria ambazo awali zilikuwa haziwezi kupatiwa misaada hiyo.

Msemaji wa UNHCR Ron Redmond amesema ghasia ziliendelea kwa kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano hayakuzingatiwa hivyo jitihada za kusambaza misaada zilikwamishwa. Lakini amesema UNHCR kwa kushirikiana na washirika wake waliweza kusambaza baadhi ya vifurushi vya misaada huko Homs, kusini mwa mji wa Hassakeh, Al Raqqa na Aleppo. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(SAUTI YA ASSUMPTA MASSOI)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031