IOM yaomba dola milioni 5.3 kuwasaidia watu waliohama makwao mashariki mwa DRC

Kusikiliza /

 

Wakimbizi wa ndani DRC

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limetoa ombi la dola milioni 5.3 kwa jamii ya kimataifa fedha ambazo zitasaidia katika utaoji wa huduma za kibinidamju kwa kati ya wakimbizi wa ndani 120,000 na 140,000 miezi mitatu inayokuja, kwenye eneo ya Orientale na katika mikoa ya Kivu kaskakzini na kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Maelfu ya raia wanaripotiwa kukimbia kambi za wakimbizi wa ndani karibu na mji wa Goma na Kivu Kaskazini wakiwemo wakimbizi 60,000 kutoka kambi ya Kanyaruchinya na wengine 30,000 kutoka kambi ya Mugunga iliyo kilomita chache kutoka mji wa Goma. Kulingana na wafanyikazi wa IOM mjini Goma ni kuwa hali ya usalama imezorota tangu waasi waudhibiti mji na kusababisha kuhama kwa watu wengi na kuongeza kwa mahitaji ya kibinadamu. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM

SAUTI YA JUMBE

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2015
T N T K J M P
« dis    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031