Homa ya manjano yazidi kusambaa jimbo la Darfur: WHO

Kusikiliza /

homa ya manjano

Shirika la afya duniani, WHO limesema idadi ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa homa ya manjano kwenye jimbo la Darfur, huko Sudan imefikia 67 huku idadi ya wagonjwa ikiongezeka maradufu kutoka 84 wakati ugonjwa huo uliporipotiwa hadi 194.

Kwa mara ya kwanza ugonjwa huo unaoenezwa na mbu, uliripotiwa mwezi Oktoba na umeshaenea katika vitongoji 17 vilivyoko maeneo ya Kati, magharibi, kaskazini na kusini mwa Darfur.

Kundi la wataalamu wa afya wa WHO na wale wa Wizara ya afya nchini Sudan limekwenda eneo hilo kusaidia kuzuia kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo.

WHO imesema inawapatia mafunzo zaidi ya wahudumu 225 wa afya huko Darfur ili wasaidie mikakati ya udhibiti, kuhudumia wagonjwa na kinga na kwamba viongozi wa maeneo hayo wameshirikishwa katika kampeni ya kuzuia kusambaa kwa homa ya manjano.

Kwa mujibu wa WHO, hakuna dawa maalum ya kutibu homa ya manjano bali chanjo ndio njia pekee ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031