Hatua zichukuliwe kutokomeza njaa katika nchi zenye ardhi kame

Kusikiliza /

Jose Graziano da Silva

Mizozo, ukame wa mara kwa mara na mfumuko wa bei ya chakula vimezinasa nchi barani Afrika na Mashariki ya Kati katika lindi la njaa, ingawa kuna njia kujinasua kutoka kwa tatizo hili- amesema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, José Graziano da Silva. Bwana da Silva amesema hayo kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu Usalama wa Chakula katika maeneo ya ukame, ambao unafanyika mjini Doha, Qatar.

Mkutano huo wa siku mbili unawaleta pamoja wawakilishi wa serikali, wasomi, mashirika ya maendeleo, wawakilishi wa umma na sekta binafsi kutoka nchi 60, ili kujadili usalama wa chakula na uwekezaji katika nchi zenye ukame.

Mkutano huo unatarajiwa kufanya mapendekezo ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa, na ambayo yatajumuishwa kwenye sera za siku zijazo, mikakati na uwekezaji ambao utaongeza uzalishaji katika kilimo, kuimarisha usalama wa chakula na uwezo wa kukabiliana na mfumuko wa bei mbeleni. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930