Hatari ya ugonjwa wa Hepatitis E inaongezeka Sudan Kusini: UNHCR

Kusikiliza /

kambi nchini Sudan Kusini

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataiafa, UNHCR, limesema kuwa uwezo wa kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa Hepatitis E nchini Sudan Kusini ni mdogo kwa sababu ya ufadhili mdogo.

Shirika hilo limeonya kuwa hatari ya maambukizi zaidi itaongezeka ikiwa idadi ya wakimbizi wanaowasili kutoka majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile katika nchi jirani ya Sudan itaongezeka, kama inavyotarajiwa.

Tayari zaidi ya watu 1000 katika kambi za wakimbizi wameambukizwa ugonjwa huo, ambao hutokana na kula chakula na maji chafu, na ambao huharibu ini, na wakati mwingine kuua. Kufikia sasa wakimbizi 26 wamefariki dunia katika kambi za jimbo la Upper Nile, idadi hiyo ikiwa imepanda kwa watu kumi zaidi tangu kati mwa mwezi Septemba. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

“UNHCR na wadau wengine tayari wanakabiliana na mlipuko wa Hepatitis E katika majimbo ya Upper Nile na Unity, ambako ugonjwa huo umeenea, na ambako wakimbizi 175, 000 wa Sudan wamepewa makazi. Hatari ya maambukizi ipo juu katika maeneo ya watu wengi, kama vile kambi za wakimbizi. Hatari hiyo inaongezeka hata zaidi katika msimu wa mvua kwa sababu ya mafuriko na uchafu. Wanawake na watoto wamo hatarini zaidi. Operesheni yetu ina uhaba wa ufadhili, na tunahitaji angaa dola milioni 20 hadi mwishoni mwa mwaka kuendeleza shughuli za kuokoa maisha.”

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031