Harakati za kuleta amani mashariki mwa DRC zaendelea

Kusikiliza /

kundi la M23

Siku ya Jumanne tarehe 20 mwezi huu iliripotiwa kuwa waasi wa kikundi cha M23 huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC waliingia na kusonga ndani ya mji wa Goma. Siku hiyo hiyo usiku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kuhusu DRC ambapo pamoja na mambo mengine limetaka waasi wa kikundi cha M23 kuondoka mara moja kwenye mji huo ulioko jimbo la Kivu Kaskazini.

Azimio hilo pia limetaka kuangaliwa uwezekano wa kuwekewa vikwazo makamanda mawili wa M23 na pia Katibu mkuu kutoa taarifa kwa Baraza la Usalama juu ya madai ya kuwepo usaidizi wa kigeni kwa M23. Azimio hilo limepitishwa wakati nchi 11 za Maziwa Makuu zikiazimia kutuma tume ya waangalizi wa kijeshi kwenye mpaka wa DRC na Rwanda katika juhudi za kumaliza mgogoro kati ya nchi hizo mbili. Waangalizi hao wa Kijeshi watakuwa na jukumu la kupalilia njia ya kikosi huru cha Walinda amani mashariki mwa DRC.

Pamoja na juhudi hizo kupiga hatua, hata hivo changamoto bado ni nyingi hasa muundo wa kikosi hicho na jinsi ya kushughulikia makundi ya wapiganaji. Mwandishi wetu Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga ametuandalia makala haya. Ungana naye.

(PKG YA RAMADHAN KIBUGA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930