Harakati za kupambana na Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu zatia matumaini: Jaramillo

Kusikiliza /

kupambana na Ukimwi

Mfuko wa kimataifa wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria umetoa taarifa mpya inayoonyesha ongezeko la idadi ya watu wanaopata dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi duniani pamoja na ikiwemo kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto.

Meneja Mkuu wa mfuko huko Gabriel Jaramillo amenukuu taarifa hiyo mpya inayoonyesha ongezeko la watu Laki Tisa kwenye idadi ya watu wanaopata dawa hizo tangu mwishoni mwa mwaka 2011, idadi ambayo inafanya watu wanaonufaika dawa zinazotolewa na mfuko huo kufikia Milioni Nne nukta Mbili.

Amesema idadi imeongezeka kutokana na upatikanaji rahisi wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi na kupungua kwa bei ya dawa hizo kwenye nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara akitolea mfano Zimbabwe na Zambia, mipango ambayo amesema inawezeshwa na mfuko huo.

Halikadhalika taarifa hiyo mpya inaonyesha maendeleo makubwa katika vita dhidi ya Malaria na Kifua Kikuu kutokana na wagonjwa zaidi kujitokeza kutibiwa kifua kikuu na watu wengi zaidi kutumia vyandarua vyenye dawa ili kujikinga na Malaria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031