Hali ya kibinadamu yazidi kudorora Syria wakati msimu wa baridi kali ukikaribia

Kusikiliza /

hali ya kibinadamu yazidi kudorora, Syria

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema kadri mzozo unavyozidi kuimarika nchini Syria, hali ya kibinadamu inazidi kudorora wakati huu ambapo idadi ya wanaohitaji misaada ya kibinadamu nchini humo ikiongezeka na kufikia watu Milioni Mbili na Nusu.

Jarida la hali ya kibinadamu linalotolewa na OCHA limesema misaada ya kibinadamu wakati wa msimu wa baridi kali unaotarajiwa kuwa na kiwango cha chini ya nyuzi joto Sifuri kwa kipimo cha Selsiyasi katika baadhi ya maeneo unalenga takribani watu Milioni Moja na Nusu na kiasi cha dola Milioni 40 zinahitajika kwa ajili ya vifaa hivyo.

OCHA imesema idadi ya wanaohitaji msaada inatarajiwa kuongezeka hususan miongoni mwa raia wa Syria waliopoteza makazi yao nchini humo ambapo watu watahitaji zaidi nguo, malazi na mazingira yenye joto ili kujisetiri na baridi

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031