Hali ya kibinadamu nchini DRC ni mbaya: OCHA

Kusikiliza /

John Ging

Mkurugenzi wa Operesheni wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa, OCHA. John Ging amezungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani na kusema kuwa hali ya kibinadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC ni mbaya wakati huu ambapo zaidi ya watu Milioni Mbili wamekimbia makazi yao ndani ya nchi hiyo

Ging amesema hayo baada ya yeye pamoja na maafisa kutoka Uingereza na Marekani na kutembelea majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini kujionea matatizo ya kibinadamu yanayowakumba wakazi wa eneo hilo kutokana na mgogoro unaoendelea.

Amesema mzozo unaosababishwa na kikundi cha M23 na vikundi vingine kadhaa vya waasi vimechochea kile alichokiita kuwa ni mahitaji makubwa ya misaada ya kibinadamu mashariki mwa DRC.

“Ukweli kwamba tuna zaidi ya watu Milioni 2.4 nchini DRC ikiwemo zaidi ya Milioni 1.6 katika majimbo ya Kivu Kusini na Kivu kaskazini, hiyo ni ushahidi mkubwa wa hali mbaya ya kibinadamu inayokabili nchi hiyo. Kadri waasi wanapoimarisha mzozo, ni wananchi wa Kivu ndio wanaoathirika. Wanaume wanauawa, wanawake wanabakwa na watoto wanalazimishwa kutumikishwa wakati vijiji vinaibwa mali zao na kuharibiwa. Lakini licha ya machungu yote haya, niligswa sana na msimamo na utu wa raia wa DRC ambao wameendelea kukabiliana na hali hiyo."

Bwana Ging amesema fedha zinahitajika haraka ili kupeleka misaada ya kuokoa maisha kwenye eneo hilo la mzozo mashariki mwa DRC.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930