Haiti yahitaji mamilioni ya fedha kwa ajili ya sekta ya kilimo iliyoharibiwa na Sandy: FAO

Kusikiliza /

mafuriko nchini Haiti

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO na serikali ya HAITI zinahitaji zaidi ya dola Milioni 74 katika kipindi cha miezi 12 ijayo kwa ajili ya kurekebisha sekta ya kilimo nchini humo iliyoharibiwa na kimbunga Sandy.

Kimbunga hicho kilichopiga mwishoni mwa mwezi uliopita kimeharibu miundombinu maeneo ya vijijini pamoja na mazao, ardhi, mifugo, mashamba ya uvuvi na kilimo na kuacha raia zaidi ya Laki Sita wa Haiti wakiwa hatarini kukumbwa na uhaba wa chakula na lishe.

FAO inasema kuwa kati ya fedha hizo zinazohitajika, dola Milioni nne zinahitajika haraka kusaidia familia elfu 20 kupanda mazao wakati wa msimu wa baridi kali unaonza mwezi ujao. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031