Ghasia zaendelea kuwalazimu watu zaidi kuhama nchini Myanmar

Kusikiliza /

myanmar-family-idp-camp1

Idadi ya watu waliolazimika kuhama makwao kutokana na ghasia za kisiasa kwenye mkoa wa Rakhine nchini Myanmar imefikia watu 110,000 kwa mujibu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA. Takriban watu 89 wameuawa tangu kuanza kwa kwa mzozo mwezi Oktoba huku zaidi ya nyumba 5,300 na maeneo ya kuabudu vikiharibiwa.

OCHA inasema kuwa hali ya usalama kwenye mkoa huo inasalia kuwa tete na watu zaidi wanatarajiwa kuhama. Jens Laerke kutoka OCHA anasema kuwa watu waliohama makwao wanahitaji kwa dharura chakula , makaoa na huduma za afya akiongeza kuwa kuifikia kambi waliko wakimbizi ni changamoto kutokana na ukosefu wa usalama.

Hali bado ni tete, serikala inafanya kila iwezalo kudhibiti hali iliyopo, lakini bado hali ni tete. Kile tunajua kutoka na mataokeo ya awali ni kuwa wanahitaji chakula, makaoa na mahitaji mangine muhimu. Bado tunatoa wito wa kufikia watu zaidi kwa kuwa watu wanazidi kuhama maeneo mengi. Kwa sababu wakati tunapohitaji kuelekea maeneo mengine pia tunahitaji usalama kweye sehemu hizo zote.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031