Biashara haramu ya ngozi ya chatu yashika kasi

Kusikiliza /

ngozi ya chatu

Utafiti mmoja umebaini kuwepo kwa ongezeko kubwa la usafirishwaji wa ngozi ya chatu inayosafirishwa kwa wingi toka Kusini mwa Asia na kupelekwa eneo la Mashariki.

Wananchi wa bara la Ulaya ndiyo wanatajwa kuhusika kwa kiwango kikubwa katika biashara ya ngozi ya chatu wanaotumia kutengeneza bidhaa zinazokwenda na wakati.

Inaelezwa kuwa kila kwama wastani wa nusu milioni ya ngozi husafirishwa kwenye eneo hilo. Utafiti huo umesema kuwa kukua kwa biashara hiyo kunazua kitisho juu ya usalama wa wanyama na hali jumla ya uoto wa asili.Kuna wasiwasi wa kuwepo uwezekano wa kupotea ngozi ya chatu.

Wakati akizindua ripoti ya utafiti huo, Mkuu wa Kituo cha biashara za kimataifa, Alexander Kasterine, alisema kuwa ripoti hiyo imefichua namna biashara isiyo halali inavyoshika kasi kwenye eneo hilo hatua ambayo ameeleza kuwa inazua hali ya wasiwasi juu ya mustakabala wa viumbe hai.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031