Bei ya chakula ilishuka kidogo mwezi Oktoba: FAO

Kusikiliza /

Bei ya chakula ilishuka kwa asilimia moja ya kipimo wastani cha Shirika la Chakula na Kilimo, FAO mnamo mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha katika kipindi cha miezi kumi ya kwanza mwaka huu, bei ya chakula ilikuwa asilimia 8 wastani, na hivyo kuwa chini ya ilivyokuwa katika kipindi sawa na hicho mwaka 2011.

Bei ya kapu la chakula ilishuka kwa pointi mbili kutoka pointi 215 hadi 213. Kushuka huku kulisababishwa hasa na bei za chini za kimataifa za nafaka na mafuta ya kupikia, ambazo mara nyingi husaidia kushusha gharama za bidhaa za ufugaji na sukari.

Wakati huo huo, ripoti ya FAO ya masoko ya kimataifa, ambayo huchapishwa mara mbili kila mwaka, imesema kuwa gharama nafuu ya bidhaa na usafirishaji kimataifa, pamoja na ununuzi mdogo wa nafaka, huenda vikalazimu gharama ya kuagiza vyakula kutoka ng'ambo kushuka hata zaidi mwaka 2012. Taarifa kamili na Joshua Mmali

TAARIFA YA JOSHUA MMALI

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031