Ban atoa wito wa kumuunga mkono Malala na elimu kwa watoto wote

Kusikiliza /

Malala Yousfzai

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa watu wote duniani kushiriki kampeni ya  kumuunga mkono mtoto wa kike wa kipakistani Malala Yousfzai aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi mwezi uliopita na watalibani kutokana na utetezi wake kwa elimu.

Katika ujumbe wake, Bwana Ban amesema tarehe 10 mwezi huu ambayo ni siku ya kampeni ya kimataifa kwa Malala, wakazi wa dunia wanatoa sauti kwa pamoja kumuunga mkono mtoto huyo wa kike na watoto Milioni 61 duniani kote ambao bado hawaendi shuleni.

“Mjumbe wangu maalum wa elimu duniani, Gordon Brown, atatoa ombi maalum la kumuunga mkono Malala pamoja na haki watoto duniani kote kupata elimu. Nami naongeza sauti yangu kwenye ujumbe wa zaidi ya watu Milioni Moja duniani. Elimu ni haki ya msingi. Ungana nasi katika kampeni ya kuipa elimu nafasi ya kwanza kwa Malala na watoto wa kike na wa kiume duniani kote."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031