Balozi Mahiga apongeza Bunge la Somalia kwa kuridhia baraza jipya la mawaziri

Kusikiliza /

Mwakiilshi maalum wa Umoja wa Mataifa huko Somalia, Balozi Augustine Mahiga na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga amesifu hatua ya bunge la Somaliaya ya kukubali na kupitisha baraza jipya la mawaziri la nchi hiyo.

Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia, UNPOS, imemkariri Balozi Mahiga akisema kuwa hiyo ni hatua muhimu na inaonyesha utashi wa uongozi wa Somali wa kuondokana na fikra za kizamani na kuleta mabadiliko chanya.

Ameonyesha kufurahishwa na uteuzi wa wanawake wawili katika baraza hilo lenye mawaziri Kumi ambapo mmoja wao Fauzia Yusuf Haji Adan anashika wadhifa wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mwanamke kushika wadhifa wa juu namna hiyo kwenye nchi za pembe ya Afrika.

Balozi Mahiga amesema ofisi yake itaendelea kushirikiana na serikali ya Somalia  kuimarisha uwezo wa serikali, kuendeleza maridhiano ya kisiasa, kuimarisha ulinzi na ujenzi wa nchi hiyo kwa mujibu wa misingi sita ya uendelezaji wa nchi hiyo iliyowekwa bayana na serikali.

Barazahilola mawaziri litaapishwa wiki ijayo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031