Nyumbani » 27/11/2012 Entries posted on “Novemba 27th, 2012”

Ban na Üzümcü waomba mataifa yote kujiunga na mkataba wa kupinga silaha za kemikali

Kusikiliza / moon_uzumcu_kane

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kupinga Silaha za Kemikali, Ahmet Üzümcü, leo wametoa waraka wa pamoja kwa nchi nane zisizo wanachama wa mkataba kuhusu silaha za kemikali. Waraka wa viongozi hao wawili unasisitiza umuhimu wa mataifa yote kutia saini mkataba wa kupinga silaha za kemikali, [...]

27/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashauriano ya dhati ndio njia pekee ya amani Mashariki ya Kati: Serry

Kusikiliza / Robert Serry, Gaza

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye mchakato wa amani huko Mashariki ya Kati, Robert Serry amesema mwendelezo wa mapigano ya kusikitisha kwenye eneo hilo inadhahirisha vile mamlaka zilizoko zisivyo na mashiko. Akitoa taarifa yake mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo mjini New York, Marekani kuhusu hali ya usalama Mashariki [...]

27/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

OCHA yaongeza fedha kwa msaada huo Rakhine; WFP yaonyesha wasiwasi wa kuendeleza msaada mwaka ujao

Kusikiliza / msaada kutoka OCHA,  Myanmar

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu OCHA kupitia mfuko wake wa utoaji misaada kwa dharura, CERF, imetoa nyongeza ya dola Milioni Tano nukta Tatu kwa ajili ya watu Elfu 36 waliopoteza makazi yao kutokana na ghasia za mwezi Oktoba kwenye jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Fedha hizo zitasaidia jitihada za mashirika matano [...]

27/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa yaweza kuwa kichocheo cha kudhibiti utoaji gesi chafuzi

Kusikiliza / permafrost inayeyuka

Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa unafanyika Doha, Qatar suala kubwa likiwa ni hatua za kuchukua kupunguza gesi chafuzi zinazochochea ongezeko la joto duniani. Wakati hilo likijdaliwa, shirika la mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, UNEP, limetoa taarifa inayozungumzia uwezekano wa kuyeyuka kwa kasi kubwa kwa udongo wenye barafu, Permafrost, ulioko kwenye maeneo [...]

27/11/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ongezeko la joto duniani huenda likawa juu zaidi udongo wenye barafu ukiyeyuka kwa kasi: UNEP

Kusikiliza / permafrost

Shirika la mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, UNEP, limeonya kuwa ongezeko la joto duniani huenda likawa juu zaidi ikiwa udongo wenye barafu ulioko kwenye maeneo ya kaskazini mwa dunia utaendelea kuyeyuka kwa kasi ya sasa. Udongo huo, uitwao Permafrost katika lugha ya Kiingereza, umeenea kwa takriban robo ya eneo lote la kaskazini mwa [...]

27/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara haramu ya ngozi ya chatu yashika kasi

Kusikiliza / ngozi ya chatu

Utafiti mmoja umebaini kuwepo kwa ongezeko kubwa la usafirishwaji wa ngozi ya chatu inayosafirishwa kwa wingi toka Kusini mwa Asia na kupelekwa eneo la Mashariki. Wananchi wa bara la Ulaya ndiyo wanatajwa kuhusika kwa kiwango kikubwa katika biashara ya ngozi ya chatu wanaotumia kutengeneza bidhaa zinazokwenda na wakati. Inaelezwa kuwa kila kwama wastani wa nusu [...]

27/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Marekebisho ya Katiba Colombia kuhusu mahakama za kijeshi yaangaliwe upya: UM

Kusikiliza / ramani ya Colombia

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya haki za binadamu, inamsihi Rais wa Colombia na kiongozi wa bunge la nchi hiyo kuangalia upya mchango wao kwenye marekebisho ya katiba ya nchi hiyo ambayo yanalenga kubadilisha wigo wa mfumo wa mahakama ya kijeshi nchini humo. Msemaji wa ofisi hiyo Cécile Pouilly amewaambia waandishi wa [...]

27/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya kibinadamu kutoa misaada zaidi kwa wakimbizi Goma: OCHA

Kusikiliza / DRC

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu yanafanya jitihada za kuwasaidia watu 140,000 kwenye sehemu 12 waliko wakimbizi wa ndani, nje na ndani mwa mji wa Goma. Shirika la Care International limeendesha tathmini kuhusu dhuluma za kijinsia kwenye kambi za wakimbizi ambapo linatarajiwa [...]

27/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya kutoa misaada yarejelea shughuli za utoaji misaada Goma: UNHCR

Kusikiliza / Goma, Congo

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na washirika wake wamerejelea shughuli zao za kuwasaidia wakimbizi wa ndani kwenye maeneo 12 mjini Goma kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambapo misaada inatolewa ikiwemo chakula, sabuni na vyombo vya maji. Usambazaji wa misaada ulianza mwishoni mwa wiki ukiwalenga watu 110,000. Hi ndiyo shughuli ya [...]

27/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA yakaribisha msaada toka Ujerumani kusaidia waathirika wa mapigano Syria

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Serikali ya Ujerumani imehaidi kutoa kiasi cha Euro milioni 12 kusaidia mfuko unaoratibu majanga ya dharura kwa Syria kiasi ambacho kimetajwa kuwa ni kunakubwa kutolewa na nchi moja. Hii ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kuhaidi kuchangia mfuko wa majanga ya dharura unaosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya utu wema [...]

27/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Fedha zahitajika kwa mipango ya kuwezesha wakimbizi wanaorejea Burundi waishi vyema: IOM

Kusikiliza / wakimbizi wa Burundi

Shirika la uhamiaji la kimataifa, IOM linasema linahitaja dola Milioni Mbili nukta Nane kwa ajili ya kusaidia mpango wa kurejea nyumbani kwa hiari kwa wakimbizi Elfu 37 wa Burundi walioko bado nchini Tanzania. Wakimbizi hao ni kati ya wakimbizi 39,700 wa Burundi waliokuwa wakiishi kwenye kambi mbili za Mtabila na Nyarugusu tangu vurugu za kikabila [...]

27/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031