Nyumbani » 26/11/2012
Entries posted on “Novemba 26th, 2012”
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema ni muhimu viongozi wa dini na wale wa kisiasa wakatumia ushawishi wao kwa maslahi ya umma huku akigusia matukio ya hivi karibuni huko Mashariki ya Kati na Mali yaliyoonyesha faida ya kuendeleza mahusiano mazuri na ya muda mrefu. Amesema mjini Vienna, Austria wakati wa uzinduzi wa [...]
26/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu kwa wakimbizi wa ndani Chaloka Beyani hii leo ameitaka serikali ya Sudan kuongeza jitihada za kupatia suluhisho la kudumu raia wake kwenye maeneo mbali mbali nchini humo waliopoteza makazi. Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku Tisa nchini Sudan iliyomkutanisha na watu kutoka pande [...]
26/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu upataji wa haki ya afya, Anand Grover amehitimisha ziara yake ya takribani wiki mbili huko Japan na kusisitiza umuhimu wa kufuatilia madhara ya miali ya nyuklia iliyotokana na ajali ya Fukushima kwa binadamu na wananchi wenyewe kushiriki kuhakikisha wanapata haki hiyo. Hata hivyo Grover amepongeza jitihada za serikali [...]
26/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi, na utamaduni UNESCO Bi Irina Bokova amesema kuwa jamii inapaswa kujengewa mustakabala bora ikiwemo pia kujengewa daraja litalounganisha utamaduni wa watu wote. Bi Bokova ambaye alikuwa akizungumza kwenye ufunguzi tamasha moja la kimataifa lililofanyika Uturuki, amesisitiza ulazima wa kuunganisha utamaduni wa mataifa . Tamasha [...]
26/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Idadi ya raia walioathiriwa na tetemeko la ardhi liliikumba Haiti miaka mitatu iliyopita,ambao bado wanaendelea kuishi kwenye makambi inakadiriwa kufikia 357,785 ikiwa imepungua kwa wastani wa asilimia 70 ikilinganishwa na takwimu za awali. Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM Gregoire Goodste anasema kuwa kiwango hicho ni hadi kufikia mwezi Octoba [...]
26/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kiasi kikubwa cha pesa zinazotumwa nyumbani na wahamiaji wafanyikazi kutoka nchini maskini zaidi duniani zinatumika kusimamia gharama ya kutuma kwa mujibu wa ripoti ya shirika la biashara na maendleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD. Ripoti hiyo inasema kuwa gharamna ya kutuma pesa kwenda kwa mataifa ya Afrika nI mara tatu zaidi kulingana nakiwango cha wastani [...]
26/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amerejelea ahadi ya shirika hilo kujitolea kukabiliana na dhuluma za ngono na kijinsia, akisema kwamba UNHCR imeongeza juhudi zake mwaka huu kuwasaidia waathiriwa kupata haki. Bwana Guterres amesema, ingawa kuna ufahamu mkubwa wa dhuluma za ngono na jinsia na juhudi za kuzipinga, [...]
26/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Huko Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada kwa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limetoa taarifa kuhusu hali halisi baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya kikundi cha Hamas na Israel na kusema makubaliano hayo yanaonekana kuzingatiwa licha ya mauaji ya mtu mmoja huko Khan Younis eneo lililoko mpakani. Kwa mujibu [...]
26/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameunga mkono taarifa ya pamoja ya Marais Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda na Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ya kuwataka waasi wa kikundi cha M23 walioingia na kusonga katika mji wa Goma, huko Mashariki mwa DRC kuacha mapigano mara moja. Msemaji [...]
26/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID umeshiriki katika kuleta maendeleo ya kielimu kwenye eneo hilo kwa kuipatia wizara ya Elimu ya Darfur Kaskazini mahema 12 yatakayokuwa madarasa kwa wafugaji wanaohamahama kwenye vitongoji vitano vya eneo hilo. Taarifa ya UNAMID imesema kuwa msaada huo ni sehemu ya miradi [...]
26/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkutano wa 18 wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa umeng’oa nanga hii leo mjini Doha Qatar. Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo rais wa vikao Abdullah Bin HamadAL-Attiyah amewaambia wanaohudhuria kuwa madadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa kwa ubinadamu na mkutano huo ni fursa muhimu inayostahili kutumika kwa njiia nzuri. [...]
26/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »