Nyumbani » 23/11/2012 Entries posted on “Novemba 23rd, 2012”

Ujumbe wa UM kuelekea Bahrain kuangalia ukiukwaji wa haki za binadamu

Kusikiliza / Rupert Colville

Jopo la Umoja wa Mataifa la kutathmini haki za binadamu, mapema mwezi ujao litakwenda Bahrain kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo kujadili mfumo wa mahakama nchini humo na uwajibikaji kwa vitendo vya sasa na vilivyopita vya ukikwaji wa haki za binadamu. Msemaji wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Rupert Colville [...]

23/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Pillay asikitishwa na kurejeshwa kwa adhabu ya kifo Afghanistan

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu, Navi Pillay ameeleza wasiwasi wake mkubwa juu ya hukumu ya kifo dhidi ya wafungwa 14 nchini Afghanistani iliyotekelezwa tarehe 20 na 21 mwezi huuu. Taarifa ya Tume ya haki za binadamu inasema kuwa Rais Hamid Karzai ameripotiwa kuidhinisha adhabu ya kifo kwa wafungwa [...]

23/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaelezea wasiwasi kuhusu elimu na afya ya watoto mashariki mwa DRC

Kusikiliza / School DRC

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa karibu wakimbizi wa ndani 140,000 wanaishi kwenye shule tatu za umma, kituo cha Don Bosco na kwa kambi tatu za wakimbizi wa ndani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. UNICEF inasema kuwa watoto wako kwenye hatari ya maradhi ya kuambukiza yakiwemo kipindupindu kutokana na [...]

23/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kufungwa uwanja wa ndege Goma kwakatiza shughuli za utoaji misaada DRC na kibinadamu: OCHA

Kusikiliza / Walinda amani wa UM na wanajeshi wa DRC

Huku hali kwenye mji wa Goma ikibaki kuwa tete , uwanja wa ndge ambao ndio tegemeo la wafanyikazi wa kutoa huduma za kibinaadamu umebaki umefungwa na kufanya utoaji wa huduma na misaada kuwa mgumu. Mapigano makali kati ya makundi ya FARDC na M23 eneo la Masisi Magharibi mwa Goma yamesababisha kuhama kwa watu zaidi . [...]

23/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dhuluma dhidi ya wanawake bado yaathiri wanawake 3 kati ya wanawake 10 duniani

Kusikiliza / Violence against Women

Huku siku ya kimataifa ya kupinga dhuluma dhidi ya wake ikitarajiwa kuadhimishwa tarehe 25 mwezi huu Shirika la afya duniani linasema kuwa bado wanawake 3 kati ya wanawake 10 wanapitia dhuluma nyingi duniani. WHO inasema kuwa dhuluma ya kimapenzi ndiyo inayotumika zaidi kama silaha. WHO Inasema kuwa hata kama upashaji tohara umepungua duniani bado watoto [...]

23/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uimarishaji kilimo Haiti wahitaji dola Milioni 74: FAO

Kusikiliza / Athari za Kimbunga Sandy Haiti

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO na serikali ya Haiti zinatafuta dola Milioni 74 katika kipindi cha mwaka mmoja ujao kwa ajili ya kurekebisha sekta ya kilimo nchini humo iliyoharibiwa na mfululizo wa majanga ya asili tangu kuanza kwa mwaka huu. Majanga hayo ni vimbunga Sandy na Isaac pamoja na ukame ambayo yamefanya Haiti [...]

23/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mijadala ya UM kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa sio tu kuhusu pesa, asema mtaalam wa UM

Kusikiliza / Mkataba wa Kyoto

  Mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa, Virginia Dandan, ametoa wito kwa serikali zote duniani ziangalie gharama ya mabadiliko ya hali ya hewa kuwa zaidi ya fedha, na kuchukua msimamo wa pamoja wa kimataifa kama sehemu muhimu ya mafanikio ya mijadala ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, ambayo itaanza wiki ijayo [...]

23/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jitihada za Malala kutetea mtoto wa Kike ziendelezwe kwa kasi kubwa: UM

Kusikiliza / Malala Yousefzai

Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema mtoto Malala Yousfzai atakuwa ametendewa haki zaidi iwapo harakati zake za kutafuta haki ya elimu kwa mtoto wa kike zitaendelezwa zaidi ya kile kilichofanywa sasa baada ya yeye kunusurika kuuawa. Katika taarifa yake kwa siku ya kimataifa ya kutokomeza aina zote [...]

23/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaomba dola milioni 5.3 kuwasaidia watu waliohama makwao mashariki mwa DRC

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani DRC

  Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limetoa ombi la dola milioni 5.3 kwa jamii ya kimataifa fedha ambazo zitasaidia katika utaoji wa huduma za kibinidamju kwa kati ya wakimbizi wa ndani 120,000 na 140,000 miezi mitatu inayokuja, kwenye eneo ya Orientale na katika mikoa ya Kivu kaskakzini na kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya [...]

23/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Misaada zaidi yahitajika Syria wakati wa baridi kali; hospitali zaharibiwa: Mashirika ya UM

Kusikiliza / watoto nchini Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema hivi sasa linakusanya zaidi ya vifurushi Laki moja vya nguo za watoto wa wakimbizi huko Syria wakati huu ambapo msimu wa baridi kali unawadia. Msemaji wa UNICEF Marixie Mercado amesema wanakusanya pia  mablanketi Laki Moja na Sitini ikiwemo ya watoto hao wa wakimbizi pamoja na [...]

23/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031