Nyumbani » 21/11/2012 Entries posted on “Novemba 21st, 2012”

Ban akaribisha usitishwaji mapigano Gaza

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekaribisha tangazo la kusitisha mapigano katika Gaza na kusini mwa Israel, na kuzipongeza pande zote katika mzozo huo kwa kufanya  hivyo, pamoja na Rais Morsi wa Misri kwa uongozi wake mzuri. Akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo limefanya kikao maalum kuhusu hali ya Mashariki [...]

21/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wanaathiriwa na machafuko yalooenea DRC: UM

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na maeneo ya vita vya silaha, Leila Zerrougui, ameelezea kusikitishwa kwake kuhusu hali ya watoto katika mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC. Kuingia kwa waasi wa M23 katika miji ya Goma na Sake, kumeambatana na ukiukaji mkubwa unaotekelezwa dhidi ya [...]

21/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

AU , FAO na Shirika la Lula waungana kuangamiza njaa barani Afrika

Kusikiliza / AU, FAO, LULA

Tume ya muungano wa Afrika pamoja na Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO kwa ushirikiano na shirika la Lula nchini Brazil wametangaza leo kuwa wataungana kusaidia kumaliza njaa na ukosefu wa lishe barani Afrika. Uamuzi huo ulafikiwa kwenye mkutano kati ya mweyekiti wa tume ya muugano wa Afrika Nkosazana Dlamini Zuma, [...]

21/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO yataka mauaji ya mwandishi wa habari huko Mexico yachunguzwe

Kusikiliza / vyombo vya habari

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova amelaani mauaji ya mwandishi wa habari Adrian Silva Moreno wa Mexico na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu chanzo cha mauaji hayo na ya afisa wa zamani wa polisi Misray López González. Bi. Bokova ambaye shirika lake lina wajibu wa kutetea [...]

21/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Bado inawezekana kuzuia viwango vya joto duniani kupanda kwa zaidi ya nyuzi 2: UNEP

Kusikiliza / mabadiliko ya hali ya hewa

Juhudi zaidi zinahitajika kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa bila kuchelewa ikiwa ulimwengu bado unataka kuwa na nafasi ya kuzuia viwango wastani vya joto kupanda kwa zaidi ya nyzui 2 katika karne hii. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, UNEP na Wakfu wa Hali ya Hewa ya [...]

21/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama la UM lapatiwa taarifa kuhusu hali ya usalama na maendeleo huko DRC

Kusikiliza / M23

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepokea ripoti ya hali ya usalama na mustakhbali wa amani na maendeleo ya kudumu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, ripoti iliyowasilishwa na Mkuu wa kikosi cha umoja wa Mataifa cha kulinda amani na kuweka utulivu nchini humo, Roger Meece.   Akiwasilisha ripoti hiyo ya Katibu [...]

21/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waomba dola milioni 41 zaidi kwa mahitaji yaloongezeka jimbo la Rakhine Myanmar

Kusikiliza / Rakhine State

  Mratibu wa masuala ya misaada ya kibinadamu nchini Myanmar, Ashok Nigam, leo amezindua mpango mpya wa kuitikia mahitaji ya dharura ya kibinadamu katika jimbo la Rakhine, Myanmar. Wakati wa uzinduzi huo, Bwana Nigam, ambaye aliandamana na waziri wa masuala ya mipaka Myanmar, Jenerali Thein Htay, ameishukuru jamii ya kimataifa kwa mchango wake kufikia sasa, [...]

21/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Programu za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi zarejelea tena nchini Mali

Kusikiliza / kupambana na ugonjwa wa Ukimwi

Mfuko wa kimataifa unaofadhili vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, Kifua kikuu na Malaria hii leo umesaini makubaliano na Shirika la maendelo la Umoja wa Mataifa UNDP ya kurejelea tena programu za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi hasa matibabu ya ugonjwa huo kwa maelfu ya watu nchini Mali. Kupitia makubaliano hayo mfuko huo uliidhinisha ufadhili [...]

21/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna mkuu wa UNRWA azuru Gaza kujioenea hali ilivyo

Kusikiliza / Filipo Grandi

Kamishina mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA Filipo Grandi ametembelea Gaza kujionea mwenyewe uharibifu uliofanywa na pia kukagua huduma za wafanyikzi wa UNRWA. Bwana Grandi amekutana na wakimbizi na kuzungumza na wafanyikazi kwenye kituo cha Jabalia ambapo alielezea kuridhika kwake na kazi inayoendelea. Bwana Grandi alisisitiza kuwa hatua [...]

21/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ashutumu shambulio dhidi ya basi huko Tel Aviv

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon ambaye yuko ziarani Mashariki ya Kati kupatia suluhu mzozo kwenye eneo hilo, ameshutumu vikali shambulio lililotokea leo kwenye basi moja huko Tel Aviv, Israel na kusababisha watu Kumi kujeruhiwa. Msemaji wa Bwana Ban, amemkariri Katibu Mkuu huyo akielezea kusikitishwa na kushtushwa na taarifa za shambulio [...]

21/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yahitaji dola Milioni 10 kukidhi huduma ya tiba huko Gaza

Kusikiliza / watoto Gaza

Shirika la afya duniani, WHO linaomba dola Milioni Kumi kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na dawa za kutumika kwenye vituo vya afya huko Ukanda wa Gaza ambako idadi ya wagonjwa imeongezeka kutokana na mapigano yanayoendelea huku vituo vya afya vikiripotiwa kushambuliwa. Mkuu wa ofisi ya WHO huko Gaza Dkt, Mahmoud Daher ameiambia Radio [...]

21/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wahitaji dola bilioni 1 kwa shughuli za misaada Sudan Kusini

Kusikiliza / sudan kusini

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa huduma za kibinadamu Sudan Kusini yamesema yatahitaji dola bilioni 1.1 za kimarekani ili kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu yanayozidi kuongezeka nchini humo mwaka ujao wa 2013. Afisi ya mratibu mkuu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema kuwa idadi kubwa ya watu Sudan Kusini bado wamo [...]

21/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM aendelea kutafiti mfumo wa udhibiti wa mipaka ndani ya EU

Francois Crepeau

Suala la udhibiti wa mipaka ya nchi za Umoja wa Ulaya litakuwa ajenda ya kipaumbele wakati wa ziara ya mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wahamiaji, François Crépeau huko Ugiriki kuanzia Jumapili ijayo. Akizungumzia ziara hiyo ya siku tisa, Crepeau amesema anakwenda Ugiriki kwa kuwa nchi hiyo imekuwa kituo muhimu kinachotumiwa na [...]

21/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930