Nyumbani » 20/11/2012 Entries posted on “Novemba 20th, 2012”

Baraza la Usalama la UM lapitisha azimio kushutumu vitendo vya M23 kuingia Goma, DRC

Kusikiliza / Waasi wa M23

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linaloshutumu vikali kitendo cha waasi wa kikundi cha M23 kuingia na kusonga ndani ya mji wa Goma huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kutishia usalama wa raia. Azimio hilo limepitishwa kwa kauli moja jumanne usiku na wajumbe wote 15 wa [...]

20/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano zaidi katika Ukanda wa Gaza hayana manufaa kwa mtu yeyote: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban na Waziri Mkuu Netanyahu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameitaka Israel kujizuia katika operesheni zake huko Ukanda wa Gaza huku akisema kuwa vifo vya raia havikubaliki katika mazingira yoyote. Bwana Ban amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Jerusalem baada ya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, mkutano ambao pia ulihudhuriwa na [...]

20/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Waasi wa kikundi cha M23 waingia mji wa Goma huko DRC: Msemaji UM

Kusikiliza / Goma displaced

Waasi wa kikundi cha M23 wameripotiwa kuingia mji wa Goma, ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Eduardo Del Buey amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani kuwa hali katika mji wa Goma sasa ni mbaya na kwamba waasi hao wamekuwa wakisonga mbele licha ya wito wa Baraza [...]

20/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua zichukuliwe kudhibiti mabadiliko ya tabianchi: Benki ya dunia

wb-warmer

Ripoti mpya kuhusu mabadiliko ya tabianchi inadokeza kuwa muda unatokomea kuweza kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi. " Turn down the Heat" au punguza kiwango cha joto, ni jina la ripoti hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya mabadiliko ya tabianchi ya Potsdam kwa ajili ya Benki ya Dunia na inaeleza kuwa kiwango cha juu cha [...]

20/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Fedha zaidi zahitajika kwa ajli ya msaada wa chakula Madagascar kabla ya kimbuga: WFP

Kusikiliza / madagascarfood

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema uhaba wa fedha ulisababisha lishindwe kuandaa kiwango cha kutosha cha msaada wa chakula kwa ajili ya wakazi wa maeneo yaliyoko kwenye mkondo wa kimbunga huko Madagascar. Msemaji wa WFP Elizabeth Byrs amesema kutokana na hali hiyo wanaomba wahisani dola Milioni Sita nukta Moja kwa ajili ya msaada [...]

20/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha mchakato wa amani Myanmar

Kusikiliza / Tomas Ojea Quintana

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu nchini Mynmar amekaribisha aamuzi wa serikali ya nchi hiyo iliyohaidi kuendesha mageuzi yenye shabaha ya kuleta usawa na kuzingatia masuala yanayohusu haki za binadamu. Tomás Ojea Quintana amesema kuwa uamuzi wa serikali ya Myanmar iliyokubali kupitia upya baadhi ya vifungu na sheria zake ikiwemo zile [...]

20/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Aung San Suu Kyi akubali jukumu la UNAIDS la kupinga unyanyapaa dhidi ya wenye Ukimwi

Kusikiliza / Aung San Suu Kyi

Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na Ukimwi, UNAIDS umemteua mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Aung San Suu Kyi kuongoza harakati za dunia za kupinga vitendo vya unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na Ukimwi. Taarifa ya UNAIDS inasema tayari Bi. Suu Kyi amekubali jukumu hilo wakati [...]

20/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukuaji endelevu na wa usawa wahimizwa kwenye siku ya viwanda Afrika

Kusikiliza / viwanda, Africa

Ukuaji endelevu, wenye usawa na ambao unawahusisha wote unahitajika ili kufikia malengo ya maendeleo ya milenia na malengo ya kichumi na kijamii ya ushirikiano wa maendeleo barani Afrika, NEPAD. Huo ndio ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, leo kwenye siku ya viwanda barani Afrika. Bwana Ban amesema mwaka huu, siku ya [...]

20/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viwango vya gesi inayochafua mazingira vyaandisha rekodi mpya mwaka 2011

Kusikiliza / gesi chafu

Kiwango cha gesi inayochafua mazingira iliyo hewani kilivunja rekodi mwaka 2011 kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo kabla ya kuanza kwa mazungumzo kuhusu mabadiliko ya mhali ya hewa juma lijalo. Shirika la utabiri wa hali wa hewa duniani WMO ambalo ndilo lilolotoa ripoti hiyo linasema kuwa kati ya mwaka [...]

20/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Maambukizi mapya ya Ukimwi yapungua kwa zaidi ya asilimia 50 kwenye nchi 25: UNAIDS

Kusikiliza / Michel Sidibe

Ripoti mpya ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na Ukimwi, UNAIDS imeonyesha kupungua kwa zaidi ya asilimia 50 ya maambukizo mapya ya virusi vya Ukimwi katika nchi 25 duniani hususan zile zilizokuwa zikiongoza kwa maambukizi mapya. Kwa mujibu wa ripoti hiyo mafanikio hayo yanatokana na kuimarishwa kwa hatua za kinga dhidi ya maambukizi [...]

20/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano yalazimu huduma za kibinadamu kusitishwa Goma, DRC

Kusikiliza / wakimbizi nchini DRC

Mashirika ya kutoa huduma za binadamu yamesitisha kwa muda oparesheni zake kwwenye maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakati mapigano yanapochacha mjini Goma na vitongoji vyake. Mashirika mengi yanayotoa huduma nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yana vituo vyao mjini Goma. Mapigano yamechacha kwa muda wa juma moja lililopita ambapo wanachama wa [...]

20/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Israeli na Hamas zisitishe mapigano na ziheshimu haki za binadamu za kimataifa:Ban

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon na Nabil Elaraby

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaendelea na ziara yake Mashariki ya Kati yenye lengo la kupatia suluhu mzozo kati ya kikundi cha Hamas na Israeli ambapo hii leo amesisitiza tena azma yake ya kuwa mapigano yanayoendelea kati ya pande mbili hizo huko Ukanda wa Gaza hayatafanya upande wowote kuwa salama. Bwana Ban amesema hayo [...]

20/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa UM wataka haki za watoto kulindwa

Kusikiliza / watoto kwenye maeneo ya vita

Wataalamu watano wa ngazi za juu katika masuala ya haki za watoto kwenye Umoja wa Mataifa wamezishauri serikali kuchukua hatua zaidi za kulinda haki za watoto kutokana na dhuluma za kila aina, kuzuia ukiukaji wa haki dhidi ya watoto na kuwafikisha mbele ya sheria wale wanao wadhulumu kimapenzi watoto na kuwatumia kwemye mizozo. Kwenye maadhimisho [...]

20/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu huko Goma vyakithiri: UM

Kusikiliza / wakazi wa Goma walohama makwao wakibeba shehena za misaada

Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama na ukiukwaji wa haki za binadamu huko Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo. Msemaji wa tume hiyo, Rupert Colville amemkariri Bi. Pillay akisema kuwa kitendo cha waasi wa M23 kusonga kwenye mji wa Goma, [...]

20/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay asikitishwa na hali ya raia walobaniwa kwenye mzozo wa Gaza

Kusikiliza / Gari la ambulance likiwachukuwa majeruhi wa Gaza hospitali

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay, ameelezea masikitiko yake kuhusu hali ya raia waliobaniwa kwenye mzozo kati ya Israel na Palestina Gaza na kusini mwa Israel. Bi Pillay ameelezea kushangazwa kwake na kuongezeka kwa idadi ya raia wa Palestina, wakiwemo wanawake na watoto, ambao wameuawa au kujeruhiwa katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita [...]

20/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031