Nyumbani » 16/11/2012 Entries posted on “Novemba 16th, 2012”

Baraza la Usalama laazimia kuongeza muda wa kikosi cha UM Abyei

Kusikiliza / baraza la usalama

Baraza la Usalama, leo kwa kauli moja limeazimia kuongeza muda wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika eneo la Abyei (UNISFA) hadi tarehe 31 Mei 2013. Eneo la Abyei lililoko kwenye mpaka kati ya Sudan na Sudan Kusini, limekuwa likizozaniwa kwa muda na nchi hizo mbili. Baraza hilo la Usalama pia limezitaka [...]

16/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi zaidi wa Sudan wawasili makazi ya Yida Sudan Kusini

Kusikiliza / yilda

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema katika kipindi cha wiki mbili sasa zaidi ya wakimbizi Elfu mbili wa Sudan wamewasili katika makazi ya Yida kukwepa mapigano nchini mwao. UNHCR limesema hivi sasa watumishi wake wanafuatilia njia ya kwenda mpakani na wanasafirisha wakimbizi walio hatarini zaidi kuelekea kambi hiyo ya Yida na [...]

16/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF Burundi yasaidia raia wanaokimbia DRC

Kusikiliza / Raia wanaokimbia DRC

  Migogoro inayoendelea sehemu mbali mbali duniani husababisha watu kutafuta hifadhi nchi za jirani kwa ajili ya usalama wao na maisha yaweze kuendelea. Barani Afrika mizozo katika nchi za maziwa makuu imefanya watu kukimbia makwao mathalani huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Katika matukio mengi wanaopata matatizo ni wanawake na watoto. Eneo la Cibitoke liko [...]

16/11/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Viwango vya UM vya haki za binadamu viwe msingi wa azimio la haki za binadamu la ASEAN

Kusikiliza / Michael Forst

Jopo kubwa zaidi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo limetaka umoja wa nchi za kusini-mashariki mwa Asia, ASEAN kuhakikisha kuwa azimio la haki za binadamu kwa eneo hilo linalotarajiwa kuridhiwa na nchi hizo kwenye kikao chao cha Jumapili huko Cambodia, linazingatia viwango vya kimataifa vya haki za binadamu. Michael Forst ambaye ni [...]

16/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ajenda ya maendeleo na mazingira zinategemeana: Mshauri wa Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Amina Mohamed

Lengo la kutokomeza umaskini halitofikiwa bila kufanya mazingira kuwa jambo la kipaumbele, kwa mujibu wa Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malengo ya Maendeleo baada ya mwaka 2015, Bi. Amina J Mohammed. Bi Mohammed amesema hayo wakati wa ziara yake kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, ambako amehutubia maafisa [...]

16/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yasaidia kukabiliana na Kipindupindu Haiti

Kusikiliza / cholera-haiti

Shirika la uhamiaji la kimataifa, IOM limechukua hatua kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu huko Haiti ulioibuka baada ya kimbunga Sandy. IOM imesema tayari imetoa takribani vitita Elfu Kumi vyenye tembe na vifaa vingine vya tiba ya ugonjwa huo ambavyo vimesambazwa wiki hii katika kambi 31 kwenye eneo la mijini na mikoa mingine huko [...]

16/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM waadhimisha miaka 60 ya huduma yake ya kutoa maelezo kwa wageni kuhusu shughuli zake

Kusikiliza / kutoa maelezo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema maelezo wanayopata wageni kuhusu shughuli za umoja huo pindi wanapotembelea makao makuu yake mjini New York, yamesaidia kutoa picha halisi na kwa wakati muafaka kuhusu chombo hicho na kuepusha taarifa zisizo sahihi. Bwana Ban amesema hayo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya shughuli ya [...]

16/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Cambodia yatuhumiwa kubinya vyama vya kiraia

Kusikiliza / HRC

Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema mwelekeo uliochukuliwa na utawala wa Cambodia katika wakati mataifa ya eneo la Asia na Pacific yakijiandaa na mkutano wa kilele wa ASEAN unatia shaka. Duru kutoka Cambodia zinasema kuwa maafisa wa serikali wamekuwa wakifuatilia kwa karibu utendaji kazi pamoja na shughuli za mashirika [...]

16/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Navi Pillay asikitika Pakistan kutekeleza hukumu ya kifo

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamshna Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay ameelezea masikitiko yake juu ya taarifa kuwa Pakistani imetekeleza kwa mara ya kwanza adhabu ya kunyonga hadi kifokatika hukumu iliyotolewa miaka minne iliyopita. Hukumu hiyo iliyotolewa mwaka 2008 na mahakama ya kijeshi dhidi ya askari mmoja ambaye alidaiwa kumua bossi wake. Taasisi za kimataifa ikiwemo kamishana ya [...]

16/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ujerumani yaipiga jeki IOM kusaidia waathirika wa mafuriko Chad

Kusikiliza / mafuriko nchini Chad

Serikali ya Ujerumani imetoa kiasi cha euro 500,000 ili kulipiga jeki shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM ambalo limechukua jukumu la kuzisaidia zaidi ya familia 38,000 zilizoathiriwa na mafuriko huko Kusin na Magharibi mwa Chad. Mafariko hayo ambayo ni mabaya kulikumba taifa hilo yamesababisha vifo vya watu 20 na kuharibu nyumba zinazokadiriwa [...]

16/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yashutumu kuhangaisha kwa watu wanaokisiwa kuwa mashoga na wasagaji nchini Cameroon

Kusikiliza / gay-cople

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi wake kutokana na ripoti za kuhangaishwa, kudhulumiwa, kukamatwa na kufungwa kwa watu wanaokisiwa kuwa wasagaji au mashoga nchini Cameroon. Sheria za sasa nchini Cameroon zinaharamisha uhusiano baina ya watu wa jinsia moja na inaruhusu hadi kifungo cha miaka mitano pamoja na faini. Sheria [...]

16/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yazinda kituo cha radio ya kijamii Kenya kusaidia utengamano kati ya wenyeji na wakimbizi

Kusikiliza / IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM leo linazindua kituo cha radio ya kijamii kwenye mji wa Kakuma, kaskazini-Magharibi mwa Kenya kwa lengo la kusaidia kuwepo utengamano miongoni mwa wakimbizi waliko kwenye kambi ya Kakuma na wenyeji wa kabila la kiturkana wanaoishi eneo hilo. Hatua hiyo inatokana na migogoro ya mara kwa mara kati ya wakimbizi [...]

16/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay alaani mashambulizi kwenye sehemu za raia kwenye ukanda wa Gaza na Israel

Kusikiliza / Faixa-de-Gaza

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa ni jambo lisilokubalika kuwa raia ndio wanaondelea kuhangaika kufuatia msukosuko uliopo kati ya serikali ya Israel na utawala wa Palestina. Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa usalama wa raia ni jukumu la pande zote husika kuambatana na [...]

16/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utoaji chanjo dhidi ya homa ya Manjano Sudan kuanza tarehe 24 mwezi huu: WHO

Kusikiliza / mbu-malaria-who

Kundi la kimataifa la kuratibu masuala ya chanjo, ICG limekubali ombi la serikali ya Sudan la kusaidia chanjo kwa ajili ya kinga dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano uliolipuka kwenye vitongoji 23 vya jimbo la Darfur. Ugonjwa huo umejikita katika maeneo ya Kati, magharibi, Kusini, Kaskazini na Mashariki mwa jimbo hilo ambapo hadi Jumanne [...]

16/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za Afrika zapatiwa mbinu mbadala ya kuepusha migogoro ya matumizi ya pamoja ya maji

Kusikiliza / water-2

Migogoro baina ya nchi za Afrika juu ya matumizi ya pamoja ya maji inaweza kupatiwa muarobaini kwa kutumia mkataba wa uhifadhi na matumizi ya pamoja ya maji ya Tume ya Umoja wa mataifa kwa masuala ya uchumi ya Ulaya, UNECE uliotumika kwa miaka 20 sasa. Mkataba huo ulijadiliwa katika kongamano la pili la Afrika kuhusu [...]

16/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031