Nyumbani » 15/11/2012 Entries posted on “Novemba 15th, 2012”

Raia walindwe dhidi ya vitendo vya ngono kwenye maeneo ya migogoro: UM

Kusikiliza / Zainab Hawa Bangura

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu unyanyasaji wa kingono katika maeneo yenye migogoro, Zainab Hawa Bangura ameshutumu vikali matukio ya kubakwa kwa wanawake na watu kukatwa viungo vyao vya siri huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC. Kauli ya Bi. Bangura inafuatia ripoti ya kuwepo kwa vitendo mbali mbali vya unyanyasaji [...]

15/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Matokeo ya uchunguzi wa yaliyojiri Sri Lanka yatasaidia kuimarisha UM: Malcorra

Kusikiliza / Susana Malcorra

Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa Susana Malcorra amesisitiza kuwa ripoti kuhusu yaliyojiri nchini Sri Lanka katika miezi ya mwisho ya vita vya wenyewe kwa wenyewe itatumiwa kuimarisha zaidi utendaji wa umoja huo hususani katika kusaidia wale wenye mahitaji. Bi. Malcorra amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani leo kuhusu ripoti [...]

15/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna mfanyakazi wa kimataifa wa UNRWA aliyeondoka Gaza

nembo ya UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada na ulinzi kwa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limekanusha madai kuwa watumishi wake wa kimataifa wanaondoka Ukanda wa Gaza. Msemaji wa UNRWA huko Gaza Adnan Abu Hasna amesema hayo huku akiongeza kuwa hali mbaya ya usalama imelazimu wasitishe shughuli zote za elimu ikiwemo kufunga shule hadi hali ya [...]

15/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Iran ifanye uchunguzi huru wa kifo cha bloga aliyekuwa kizuizi: UM

Kusikiliza / Sattar Beheshti

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limetaka Iran kufanya uchunguzi huru na wa kina usioegemea upande wowote kuhusu kifo cha bloga mashuhuri Sattar Behesthi kilichotokea akiwa kizuizini na uchunguzi huo uangalie madai ya kuwepo kwa utesaji na ripoti iwekwe hadharani. Mmoja wa wataalamu hao huru wanaochunguza haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na utesaji [...]

15/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa waadhimisha siku ya falsafa duniani

Kusikiliza / Siku ya Falsafa Duniani

  Leo ni siku ya falsafa duniani, siku inayosherekewa na Shirika la elimu , Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kila tarehe 15 mwezi Novemba. Kauli mbiu ya siku ya mwaka huu ni "vizazi vijavyo". Kwenye makao makuu mjini Paris UNESCO inatarajiwa kupanga majadiliano kuhusu vizazi vijavyo na vijana. Vizazi vijavyo ndiyo itakuwa [...]

15/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania waanza safari ya kurejea nyumbani

Kusikiliza / raia wa Burundi

Wakimbizi wa Burundi walioko nchini Tanzania katika kambi ya Mtabila wameanza kurejea nyumbani kutii agizo lilitolewa na serikali ya nchi hiyo ambayo inakusudia kuifunga kambi hiyo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Hadi sasa kiasi cha wakimbizi wapatao 8,9994 wameondoka kwenye kambi hiyo iliyoko mkoani Kigoma na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR [...]

15/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ahimiza uchaguzi wa amani Sierra Leone

Kusikiliza / uchaguzi nchini Sierra-Leone

Katika ujumbe mwingine, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa raia wa Sierra Leone wahakikishe kuwa moyo wa amani ambao umekuwepo katika harakati za uchaguzi kufikia sasa, utadumishwa hata kwenye siku ya uchaguzi, kuhesabu kura na wakati matokeo yatakapotangazwa. Taifa la Sierra Leone linajiandaa kufanya uchaguzi wa tatu tangu kumalizika vita [...]

15/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wataka machafuko yakomeshwe katika mzozo wa Israel na Palestina

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezea kusikitishwa kwake kuhusu hali inayozidi kuzorota kusini mwa Israel na Ukanda wa Gaza, na ambayo imehusisha makombora kurushwa kiholela kutoka Gaza yakiilenga Israel, na mauaji ya kulenga ya mwanajeshi wa Hamas na jeshi la Israel. Bwana Ban amerejelea ujumbe wake wa kulaani vikali mashambulizi ya makombora [...]

15/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya vifo na wagonjwa kutokana na homa ya Manjano Darfur yaongezeka: WHO

Kusikiliza / homa ya manjano

Idadi ya vifo vitokanavyo na homa ya manjano huko Darfur, Sudan imeongezeka na kufikia 110 huku idadi ya wagonjwa nayo pia ikiongezeka na kufikia 374. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani, WHO ambalo katika ripoti yake kuhusu hali halisi ya ugonjwa huo hadi juzi inaonyesha kuwa ugonjwa huo umeenea katika vitongoji [...]

15/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yataja mataifa matano kwenye orodha ya mataifa 32 yanayokiuka haki ya kuhusiana

Kusikiliza / nembo ya ILO

Shirika la kazi duniani ILO limeyataja mataifa ya Argentina, Cambodia, Ethiopia, Fiji na Peru kama mataifa yanayokiuka zaidi haki ya kuhusiana kwenye orodha ya nchi 32 zinazotajwa kuwa zinazokiuka haki ya watu kuhusiana. Kamati ya ILO inayohusika na masusla ya haki ya kuhusiana ilichunguza masuala yanayohusu haki za waajiri na vyama vya wafanyikazi za kupanga [...]

15/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania waendelea kurejea nyumbani: UNHCR

Kusikiliza / Burundi refugees Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema zoezi la kurejesha makwao wakimbizi wa Burundi walioko kwenye kambi ya Mtabila nchini Tanzania linatia moyo ambapo wakimbizi wanajitokeza kwa hiari kutii agizo la serikali ya Tanzania la kuwataka warejee makwao kwa kuwa inakusudia kufunga kambi hiyo mwishoni mwa mwaka huu baada ya amani kurejea [...]

15/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Viwango vilivyowekwa kupunguza gesi chafuzi havijafikiwa: UNEP

Kusikiliza / Gesi chafu

  Katika hatua nyingine, UNEP wiki ijayo itatoa ripoti yake mpya zaidi juu tofauti ya viwango vya utoaji wa gesi chafuzi duniani, ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi huko Doha, Qatar. Ripoti hiyo inaweka bayana kuwa viwango vya utoaji gesi chafuzi zinazoharibu tabaka [...]

15/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ripoti mpya yaonyesha uhusiano kati ya maliasili na uwezo wa nchi kukopesheka: UNEP

Kusikiliza / UNEP_logo-298x300

Ripoti mpya iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira, UNEP na washirika wake imebaini uhusiano kati ya uthabiti wa kiuchumi wa nchi ikiwemo uwezo wake wa kulipa au kurejesha madeni na uharibifu wa maliasili kama vile misitu, mazao ya samaki na ardhi. Ripoti hiyo itakayowasilishwa Jumatatu ijayo wakati wa tukio maaluum huko [...]

15/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031