Nyumbani » 14/11/2012 Entries posted on “Novemba 14th, 2012”

Fedha zaidi zahitajika kukidhi mahitaji ya kibinadamu nchini Syria: OCHA

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA limesema kadri siku zinavyosonga, mahitaji ya kibinadamu nchini Syria yanaongezeka huku uwezo wa kifedha kukidhi mahitaji hayo ukipungua. Toleo la leo la jarida la masuala ya kibinadamu la OCHA, limesema watu Milioni nne nchini Syria watahitaji misaada ya kibinadamu mapema mwakani, iwapo hali ya [...]

14/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi wa UM waliokufa wakiwa kazini wakumbukwa

Kusikiliza / annual

Umoja wa Mataifa hii leo umefanya kumbukumbu ya mwaka kwa wafanyakazi wake waliokufa wakiwa kazini ambapo kipindi husika ni kati ya Novemba Mosi mwaka jana hadi Novemba 30 mwaka huu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliongoza shughuli hiyo akiungwa mkono na Rais wa Baraza kuu la Umoja huo na yule wa Baraza [...]

14/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa ionyeshe inajali eneo la Sahel: Mjumbe wa UM

Kusikiliza / Romano Prodi

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ukanda wa Sahel barani Afrika, Romano Prodi amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuonyesha kuwa inajali eneo hilo ambalo linakumbwa matatizo lukuki ikiwemo ukame, njaa na mzozo huko Mali. Prodi ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani wa Italia amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari juu [...]

14/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa ionyeshe inajali eneo la Sahel: Romano

Kusikiliza / Romano Prodi

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ukanda wa Sahel barani Afrika, Romano Prodi amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuonyesha kuwa inajali eneo hilo ambalo linakumbwa matatizo lukuki ikiwemo ukame, njaa na mzozo huko Mali. Prodi ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani wa Italia amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari juu [...]

14/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalam wa UM ahofia vitisho dhidi ya majaji Sri Lanka

Kusikiliza / Gabriela Knaul

Mtaalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na wanasheria, Gabriela Knaul, leo ameelezea wasiwasi wake kuhusu ripoti za vitisho dhidi ya majaji na maafisa wa sheria nchini Sri Lanka, na kuonya kuwa huenda vitisho hivyo vikawa miongoni mwa mashambulizi na ulipizaji kisasi wanaokumbana nayo wanasheria. Bi Knaul amesema vitisho hivyo ni sehemu ya [...]

14/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hatua zichukuliwe kutokomeza njaa katika nchi zenye ardhi kame

Kusikiliza / Jose Graziano da Silva

Mizozo, ukame wa mara kwa mara na mfumuko wa bei ya chakula vimezinasa nchi barani Afrika na Mashariki ya Kati katika lindi la njaa, ingawa kuna njia kujinasua kutoka kwa tatizo hili- amesema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, José Graziano da Silva. Bwana da Silva amesema hayo kwenye mkutano wa kimataifa [...]

14/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vita dhidi ya ulanguzi wa watu ni wajibu wa kila mmoja:Ezeilo

Kusikiliza / Joy Ngozi Ezeilo

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Joy Ngozi Ezeilo amezitaka biashara kote duniani kuacha kutumia wafanyikazi wanaosafirishwa kiharamu na pia kuchunguza na kuzuia wafanyikazi kama hao wanaotumia wa washirika wao. Bi Ezeilo amesema kuwa katika ulimwengu wa sasa ulanguzi wa binadamu unapatikana kwenye sekta zote zikiwemo za kiuchumi na unaathiri mataifa yote yakiwemo wanakotoka , [...]

14/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uwepo wa njia za kupanga uzazi ni suala muhimu la haki za binadamu:UNFPA

Kusikiliza / kupanga uzazi

Zaidi ya wanawake milioni 220 hawana uwezo wa kufikia njia za kupanga uzazi wanazojichagulia kwa mujibu wa mfuko wa idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa (UNFPA). Shirika hilo linasema kuwa ukosefu au kutopatikana kwa njia za kupanga uzazi vimesababisha wanawake na familia zao kutumbukia kwenye umaskini, kuwa na afya duni na kukabiliwa na ubaguzi [...]

14/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waasi Mashariki mwa DRC waripotiwa kuua raia wakiwemo watoto: UM

Kusikiliza / northkivu

Takribani raia 264 wakiwemo watoto 83 wameuawa na vikundi vya waasi wenye silaha huko Mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, kati ya mwezi Aprili na Septemba mwaka huu. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Ofisi ya Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ambayo iliendesha uchunguzi wake na kubaini kuwa kikundi [...]

14/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Kisukari ni tishio kwa malengo ya maendeleo ya Milenia, tushirikiane kuutokomeza: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika ujumbe wake wa siku ya kupambana na ugonjwa wa Kisukari hii leo amesema ugonjwa huo ni changamoto kwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea na unazidi kusambaa kila mwaka kutokana na ongezeko la mifumo ya maisha isiyo ya kiafya pamoja na uzee. Amesema familia maskini zenye mgonjwa wa [...]

14/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yatabiri kuendelea kuongezeka kwa wagonjwa wa Kisukari duniani

Kusikiliza / ugonjwa wa kisukari

Wakati leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na ugonjwa wa Kisukari, Shirika la afya duniani linasema kuwa watu Milioni 347 duniani kote wanasumbuliwa na aina ya kwanza ya ugonjwa wa kisukari. WHO imesema mwaka 2004 watu Milioni 3.4 walikufa kutokana na ugonjwa wa kisukari ambapo zaidi ya asilimia 80 ya vifo hivyo ni katika [...]

14/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930