Nyumbani » 13/11/2012 Entries posted on “Novemba 13th, 2012”

Itifaki ya kudhibiti biashara haramu ya bidhaa za tumbaku yapitishwa huko Seoul: WHO

matumizi ya bidhaa za tumbaku

Kumekuwa na hali ya matumaini juu ya mpango wa kukabiliana na wimbi la matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku na biashara haramu ya bidhaa za zao hilo ambapo mataifa wanachama wa shirika la afya duniani yanayokutana huko Seoul Korea Kusini yameridhia itifaki ya kupinga biashara hiyo. Dkt. Haik Nikogosian ambaye anaongoza kitengo cha Umoja wa [...]

13/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu la UM laitaka Marekani ifute vikwazo dhidi ya Cuba

Bruno-Rodriguez-Parrilla

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo limepitisha azimio la kuitaka Marekani kufuta vikwazo vyake ilivyoiwekea Cuba mwaka 1962. Nchi 188 kati ya 193 wanachama wa Baraza hilo leo walipiga kura kuunga mkono azimi hilo huku nchi Tatu ambazo ni Marekani yenyewe, Israel na Palau zikilikataa huku visiwa vya Marshal na shirikisho la Micronesia [...]

13/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Balozi Mahiga apongeza Bunge la Somalia kwa kuridhia baraza jipya la mawaziri

Mwakiilshi maalum wa Umoja wa Mataifa huko Somalia, Balozi Augustine Mahiga na Rais wa Somalia  Hassan Sheikh Mohamud.

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga amesifu hatua ya bunge la Somaliaya ya kukubali na kupitisha baraza jipya la mawaziri la nchi hiyo. Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia, UNPOS, imemkariri Balozi Mahiga akisema kuwa hiyo ni hatua muhimu na inaonyesha utashi wa uongozi wa Somali wa [...]

13/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WHO yasema homa ya manjano yakithiri Darfur: serikali yaomba msaada wa chanjo

homa ya manjano

Wizara ya afya nchini Sudan, imelitaarifu shirika la afya duniani, WHO juu ya mlipuko wa ugonjwa wa homa ya manjano kwenye vitongoji 23 vya jimbo la Darfur ambapo hadi Jumamosi iliyopita, kulikuwepo na wagonjwa 329 ikiwemo vifo 97. WHO imesema maeneo ya kati na kusini mwa jimbo hilo la Darfur yameripotiwa kuwa na wagonjwa wengi [...]

13/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Upatikanaji wa chakula, uwezo wa kipato, changamoto kuu zinazokabili Haiti

Haiti

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limesema kuwa zaidi ya raia milioni 1.5 wa Haiti wapo hatarini kukubwa na tatizo la ukosefu wa chakula na limetaka kuchukuliwa kwa hatua za haraka kukwamua kadhia hiyo. Shirika hilo limesema kuwa hali iliyojitokeza hivi karibuni ya mabadiliko ya hali ya hewa iliyoenda na ukame [...]

13/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM watoa ombi la msaada kufadhili huduma za kibinadamu nchini Haiti

WFP

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema kuwa athari za kimbunga Sandy kwenye taifa la Haiti zilikuwa juu zaidi ya ilivyotarajiwa. Shirika hilo limesema mwitikio wa dharura wa sekta mbalimbali unahitajika, ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu, na kuepukana na janga la njaa na utapia mlo, ambavyo kwa jumla ni hatari [...]

13/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu maalum wa UM kutembelea Sudan kutathmini hali ya kibinadamu

Chaloka Beyani

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa Chaloka Beyani kesho ataanza ziara ya siku Tisa nchini Sudan kuangalia hali halisi ya raia waliojikuta wakimbizi ndani ya nchi yao. Ziara hiyo ya Beyani ambaye amepewa jukumu na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza madhila ya watu ambao ni wakimbizi ndani ya nchi zao [...]

13/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya ‘Mimi pia ni mhamiaji’, Afrika Kusini: IOM

IOM logo

Nchini Afrika kusini, Shirika la Uhamiaji la kimataifa, IOM kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wanaanzisha kampeni iitwayo, Mimi pia ni mhamiaji yenye lengo la kuhamasisha raia wa nchi hiyo wafahamu kuwa wahamiaji nao pia ni sehemu ya jamii yao na hivyo kuleta utangamano miongoni mwa wakazi wote. Kampeni hiyo itaendelea [...]

13/11/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Pillay aisifu Indonesia kwa kuridhia mikataba ya haki za binadamu lakini ataka itekelezwe nyumbani

Navi Pillay

  Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ameisifu serikali ya Indonesia kwa kuridhia mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu haraka, na wakati huohuo kuitaka itekeleze mikataba hiyo nyumbani. Bi Pillay, ambaye amekuwa kwenye ziara rasmi nchini Indonesia tangu Jumapili, amesema kuwa ameridhishwa kwa kuona kuwa harakati za kuzitafsiri [...]

13/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vifaa vya msaada kwa ajili ya raia wa Syria vyaharibiwa katika shambulio

wfp-syria-201103

Nchini Syria matukio mawili ikiwemo shambulio la bomu na utekaji nyara nchini yamesababisha kuharibiwa kwa vifaa vya misaada vilivyokuwa visambazwe kwa raia wa nchi waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema katika tukio la kwanza mablanketi Elfu Kumi na Tatu yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye ghala la shirika [...]

13/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanaokimbia ghasia Myanmar wazama kwenye Ghuba ya Bengal nchini Myanmar

ghuba ya Bengal

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Umoja wa Wataifa UNHCR limeelezea wasi wasi kutokana na mikasa ya hivi majuzi kwenye Ghuba ya Bengal iliyowakumba watu waliokuwa wakikikimbia ghasia nchini Myanmar. Kwa muda wa majuma mawili yaliyopita kumekuwa na ripoti za kuzama kwa mashua mbili kwenye ghuba ya Bengal zikiwa na takriban watu 240 kutoka [...]

13/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ushiriki wa wakulima wadogo ni muhimu ili kufanikisha vitegauchumi vya kigeni: FAO

FAO

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO limetoa ripoti mpya inayosema kuwa mipango yoyote ya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya kilimo katika nchi zinazoendelea inapaswa kufanywa kwa umakini bila kuwaengua wakulima wadogo. Ripoti hiyo iliyochapishwa leo inahusu mwelekeo na athari za vitegauchumi vya kigeni vya kilimo kwa nchi zinazoendelea na inasema kuwa [...]

13/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya "Mimi pia ni mhamiaji" yaanzishwa Afrika Kusini: IOM

ramani ya Afrika ya Kusini

Nchini Afrika kusini, Shirika la Uhamiaji la kimataifa, IOM kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wanaanzisha kampeni iitwayo, Mimi pia ni mhamiaji yenye lengo la kuhamasisha raia wa nchi hiyo wafahamu kuwa wahamiaji nao pia ni sehemu ya jamii yao na hivyo kuleta utangamano miongoni mwa wakazi wote. Kampeni hiyo itaendelea [...]

13/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930