Nyumbani » 09/11/2012 Entries posted on “Novemba 9th, 2012”

Ban atoa wito wa kumuunga mkono Yousfzai Malala

09/11/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Adhari zinazowakumba wafanyakazi wa ukusanyaji damu nchini Tanzania

Kusikiliza / ukusanyaji damu

Mara kwa mara, watu wengi hujipata wakihitaji kuongezewa damu kwa dharura. Mara nyingi, wengi huwa wamepungukiwa damu mwilini kwa sababu mbali mbali, zikiwemo ajali zinazosababisha uvujaji damu, au hata wakati wanapofanyiwa upasuaji hospitalini. Lakini ili kuongezewa damu mwilini, damu anayoongezewa mtu inapaswa kuwa salama, yaani bila magonjwa ya kuambukiza, yakiwemo magonjwa hatari kama UKIMWI. Lakini [...]

09/11/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi wanachama wa WHO zapiga hatua kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Kusikiliza / Makao Makuu ya WHO

Mfumo wa kwanza wa aina yake duniani wa kufuatialia baadhi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanayoongoza duniani kwa vifo umeridhiwa huko Geneva, Uswisi na nchi wanachama wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO. Mwenyekiti wa mkutano huo Dkt. Bjørn-Inge Larsen amesema mfumo huo umeweka malengo Tisa na viashiria 25 vya kuzuia na [...]

09/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atoa wito wa kumuunga mkono Malala na elimu kwa watoto wote

Kusikiliza / Malala Yousfzai

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa watu wote duniani kushiriki kampeni ya  kumuunga mkono mtoto wa kike wa kipakistani Malala Yousfzai aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi mwezi uliopita na watalibani kutokana na utetezi wake kwa elimu. Katika ujumbe wake, Bwana Ban amesema tarehe 10 mwezi huu ambayo ni siku ya kampeni [...]

09/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM kukagua hatua za serikali ya Tunisia kuendeleza haki

Kusikiliza / Pablo de Greiff

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa, Pablo de Greiff, ataizuru Tunisia tokea kesho Novemba 10 hadi 16, ili kufuatilia hatua zilizochukuliwa na serikali kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu zamani na kuendeleza mfumo wa haki baada ya mabadiliko. Ziara hiyo ndiyo ya kwanza kufanywa na mtaalam huru ambaye ameteuliwa na Baraza la Haki za Binadam [...]

09/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jitihada zaendelea kupata chanjo ya numonia itokanayo na bakteria na kirusi: WHO

Kusikiliza / chanjo ya pneumonia

Katika kuelekea kuadhimisha siku ya numonia duniani tarehe 12 mwezi huu, Shirika la afya WHO limesema kwa sasa kuna chanjo ya numonia inayosababishwa na bakteria pekee wakati asilimia 30 ya visa vya numonia duniani ni mchanganyiko wa maambukizi ya bakteria na virusi. Tarik Jasarevic ambaye ni msemaji wa WHO ameeleza kuwa kutokana na hali hiyo [...]

09/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kimbunga Sandy ni fundisho la kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu madhara ya kimbunga Sandy kilichokumba maeneo ya Caribbean na pwani ya Mashariki ya Marekani mwishoni mwa mwezi uliopita na kusema kuwa mataifa yatumie kimbunga hicho kuwa fursa ya kuangalia upya mambo yanayochangia mabadiliko ya tabia nchi. Pamoja na kuelezea [...]

09/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM yaipiga jeki Papua New Guinea

papua_new_guinea

Kisiwa cha Papua New Guinea kinatazamia kuboresha vitengo vyake vinavyohusika na uhamiaji pamoja na ustawi wa kiraia kufuatiwa kuzinduliwa kwa mpango mpya wa kitaalamu unaoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM. Kuzinduliwa kwa mpango huo kunafuatia mkutano uliofanyika juma hili ukiwakutanisha wataalamu wa ngazi za juu kutoka pande zote waliokutana katika [...]

09/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Raia wengi wa Sri Lanka waliokwenda nje wana matatizo ya kiafya:IOM

Kusikiliza / nembo ya IOM

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamianji IOM limefichua kile ilichokieleza kukithiri kwa vitendo korofi vilivyowaandama raia wa Sri Lank walioenda nchi za nje kwa ajili ya kusaka kazi. Ripoti hiyo imesema kuwa kiasi kikubwa cha raia hao sasa wamepatwa na magonjw ambalimbali na wengine kupoteza maisha kwa kujinyonga na kufariki kwa [...]

09/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu milioni 7.7 wameathiriwa na mafuriko Nigeria

Kusikiliza / mafuriko Nigeria

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema mafuriko nchini Nigeria yameathiri zaidi ya watu milioni 7.7. Mafuriko hayo ambayo yameelezewa kuwa mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 40, yamesemekana kuwaua zaidi ya watu mia tatu, huku wengine zaidi ya milioni mbili wakiwa wamejiandikisha kama wakimbizi wa ndani. Shirika la Afya Duniani, WHO limesema visa vya maambukizi [...]

09/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa WFP ahitimisha ziara yake Mashariki ya Kati na kuahidi msaada kwa wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / Ertharin Cousin

Katika hatua nyingine mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP Ertharin Cousin amehitimisha ziara yake ya siku tatu huko Mashariki ya Kati iliyompeleka hadi nchi za Lebanon na Jordan kujionea hali halisi ya wakimbizi wa Syria waliokimbia nchi yao kutokana na mapigano yanayoendelea. Pamoja na kuzungumza na viongozi, alikutana pia na wakimbizi mathalani [...]

09/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu yaendelea kuzorota Syria huku ghasia zikiongezeka

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Hali ya kibinadamu imezidi kuzorota huku machafuko nchini Syria yakiwa yameongezeka, kwa mujibu wa mratibu wa huduma za kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika kanda ya Mashariki ya Kati, Radhouane Nouicer, wakati wa kongamano la kibinadamu kuhusu Syria, ambalo linaendelea mjini Geneva, Uswisi. Afisa huyo wa Umoja wa mataifa amewaambia waandishi wa habari kwamba mahitaji [...]

09/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM na wataalam wajadili suluhisho la lishe bora kwa watoto

Kusikiliza / lishe kwa watoto

Mkutano wa aina yake uliofanyika wiki hii kwenye mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa umeimarisha jitihada za kuendeleza hatua za lishe bora kwa watoto kwa mujibu wa mkakati wa kuondoa njaa kwa watoto uitwao REACH. Wataalamu na maafisa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kutoka nchi 12 zinazotekeleza mpango huo wa REACH, pamoja na Ethiopia [...]

09/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hatari ya ugonjwa wa Hepatitis E inaongezeka Sudan Kusini: UNHCR

Kusikiliza / kambi nchini Sudan Kusini

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataiafa, UNHCR, limesema kuwa uwezo wa kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa Hepatitis E nchini Sudan Kusini ni mdogo kwa sababu ya ufadhili mdogo. Shirika hilo limeonya kuwa hatari ya maambukizi zaidi itaongezeka ikiwa idadi ya wakimbizi wanaowasili kutoka majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile katika nchi jirani [...]

09/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kujadili athari za itifaki ya soko la pamoja la EAC kwa uhamiaji kufanyika Tanzania: IOM

Kusikiliza / nemba ya EAC

Shirika la Kimataifa la uhamiaji kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania wiki ijayo wataandaa mkutano wa mashauriano kuhusu athari za uhamiaji zitokanazo na itifaki ya soko la pamoja la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC. Mkutano huo wa siku tatu utakaoanza jijini DSM tarehe 13 utajumuisha maafisa wa IOM, na wale wa kutoka wizara [...]

09/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031